Katibu Mkuu wa Wizara ya Biashara na Maendeleo ya Viwanda Zanzibar Dkt. Habiba Hassan Omar, amefanya ziara katika Ofisi za Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) na kukagua maandalizi ya Maonesho ya Jubilei ya Miaka 50 ya Biashara ya Kimataifa Dar es Salaam (Sabasaba). Katika ziara hiyo, Katibu Mkuu alieleza kuridhishwa kwake na hatua zilizofikiwa hadi sasa na kufafanua umuhimu wa ushiriki wa wadau katika maonesho hayo makubwa.
Aidha, Dkt. Habiba alipata nafasi ya kuzungumza na Kamati ya Kitaifa ya Ulinzi na Usalama, ambayo inaratibu masuala ya kiusalama wakati wa kipindi chote cha maonesho. Mazungumzo hayo yalilenga kuhakikisha maandalizi ya Sabasaba yanakwenda sambamba na viwango vya usalama na uratibu wa kitaifa.
Kwa upande wa TanTrade, Mkurugenzi Mkuu Dkt. Latifa M. Khamis alieleza hatua zilizofikiwa katika maandalizi, ikiwemo uandaaji wa maeneo ya maonesho na programu maalum zitakazofanyika wakati wa maonesho ili kuonesha upekee wa Maonesho ya Jubilei ya Miaka 50 tofauti na yaliyopita. Maonesho haya yanatarajiwa kufanyika kuanzia tarehe 28 Juni hadi 13 Julai 2026 katika Uwanja wa Maonesho wa Mwalimu J.K. Nyerere, Barabara ya Kilwa, Dar es Salaam















0 comments:
Post a Comment