Nafasi Ya Matangazo

September 09, 2025

Makamu Mkuu wa Chuo, Prof. Lughano Kusiluka, akikagua kwa makini uchimbaji msingi katika moja wapo ya majengo yanayoendelea kujengwa Njombe.
Mshauri Elekezi, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ufundi ya Ujenzi wa Kampasi ya UDOM, Njombe, Mhandisi Filbert Shayo (kushoto) akiwa na Mhandisi Stella Kyabula, Mkurugenzi wa Miliki na Ujenzi, wakikagua maendeleo ya Mradi wakati wa ziara.
Wawawakilishi wa Wananchi waliojumuika na Kamati ya Ujenzi wa Kampasi ya Chuo Kikuu cha Dodoma Njombe, wakikagua ujenzi unaoendelea katika viwanja vya Njosi, Njombe wakati wa ziara ya Makamu Mkuu wa Chuo. 

Mafundi wakiendelea na zoezi la kusuka Nondo kwa ajili ya Msingi kwenye jengo la Utawala linaloendelea kujengwa.
Ujenzi ukienda kwa pamoja na usomaji ramani na michoro. Watalaamu wakiangalia kwa makini michoro ya ujenzi wakati wa ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi.
Wataalamu wa ujenzi, wananchi na uongozi wa Juu wa Chuo Kikuu cha Dodoma, wakipata taarifa ya maendeleo ya ujenzi unaoendelea Njombe.
Mafundi wakiendelea na hatua za ujenzi katika jengo la bweni la wanafunzi, linalojengwa Njombe. Mradio huu unatekelezwa na Mkandarasi Dimetoclasa Realhope Ltd. Jengo hili kwa sasa linaendelea na hatua ya ujenzi wa msingi kama linavyoonekana katika picha. 
*********
Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), Profesa Lughano Kusiluka, leo Septemba 9, 2025, ametembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi wa Kampasi ya UDOM mkoani Njombe.

Profesa Kusiluka amesema ameridhishwa na hatua zilizofikiwa, lakini akamtaka mkandarasi kuongeza kasi ya ujenzi ili majengo yakamilike ifikapo Mei 2026, kama ilivyopangwa bila kuongeza muda.

Mshauri Elekezi wa Mradi, Mhandisi Filbert Shayo, amesema ujenzi umefikia asilimia 15 na hatua za msingi zinaendelea kukamilishwa.

Kampasi hiyo inatarajiwa kuwa chachu ya kuboresha elimu ya juu na kuchochea maendeleo ya kiuchumi nchini.
Posted by MROKI On Tuesday, September 09, 2025 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo