Nafasi Ya Matangazo

September 25, 2025


Matukio ya Mgombea mwenza wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa nafasi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Emmanuel John Nchimbi za mkutano wake wa hadhara wa Kampeni uliofanyika katika uwanja wa Isele, Ilula wilaya ya Kilolo mkoani Iringa,leo Alhamis Septemba 25,2025.

Dkt.Nchimbi ameendelea kupasua anga kusaka Kura za ushindi wa kishindo kwa Chama Cha Mapinduzi (CCM) ,kuelekea uchaguzi mkuu wa Oktoba 29 mwaka huu.

Pamoja na kuwahutubia Wanachi katika mkutano huo,Dkt.Nchimbi pia alitumia nafasi hiyo kumnadi mgombea Ubunge wa jimbo la Kilolo,Ndugu Ritta Kabati ,Wagombea Ubunge wa mkoa huo pamoja na Madiwani.

Dkt. Nchimbi anaendelea kunadi sera na Ilani ya CCM ya mwaka 2025 - 2030 sambamba na kusaka kura za  ushindi wa kishindo za Mgombea urais wa chama hicho, Dkt. Samia Suluhu Hassan, Wabunge na Madiwani.






Mgombea Mwenza wa Kiti cha Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupita CCM Balozi Dkt Emmanuel John Nchimbi, amesema Serikali ya Chama hicho inakusudia kuanzisha mradi mpya wa Maji utakao nufaisha maeneo ya Pawaga, mgama na Kitapilimwa katika Jimbo la Isimani.

Dkt Nchimbi ametoa ahadi hiyo leo Septemba 25, 2025 akiwa katika mkutano wa kampeni Uliofanyika Jimbo la Isimani mkoani Iringa, ambapo akiwa hapo ametumia nafasi hiyo kumuombea kura Dkt Samia Suluhu Hassan kuelekea Oktoba 29 mwaka huu.

"Lakini Vile vile endapo mkitupa ridhaa ya kuongoza Serikali, tunaahidi ujenzi wa visima vingine vipya virefu vya Maji Vitano" amesema Balozi Dkt Nchimbi.
Posted by MROKI On Thursday, September 25, 2025 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo