Nafasi Ya Matangazo

September 14, 2025










MGOMBEA Mwenza wa Kiti cha Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Emmanuel John  Nchimbi, amepokewa kwa shangwe na Wananchi Kata ya Ndungu, Jimbo la Same Mashariki,alipowasili katika uwanja wa kata hiyo  kwenye mkutano wake wa mwisho wa kampeni Mkoani Kilimanjaro leo Jumapili Septemba 14,2025.

Dkt.Nchimbi aliwanadi Wagombea Ubunge wa Mkoa huo akiwemo Mgombea Ubunge wa Jimbo la Same Mashariki,Ndugu Anne Kilango Malecella pamoja na Madiwani.

Mkutano huo ulihudhuriwa pia na Waziri Mkuu na Makamu Wa Rais mstaafu Mzee John Samuel Malecela ambaye ni mume wa Mama Anne Kilango.
Posted by MROKI On Sunday, September 14, 2025 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo