Wasafirishaji wa abiria kwa kutumia pikipiki katika eneo la kijiwe cha Mahenje Wilaya ya Mbozi Mkoani Songwe wamepewa elimu kuhusu umuhimu wa kushirikiana na Jeshi la Polisi kwa kutoa taarifa mapema kuhusu viashiria vyovyote vya uvunjifu wa amani.
"Natoa wito kwa madereva wa pikipiki na wananchi wote kwa ujumla wa kata ya Mahenje kushirikiana kwa karibu na Jeshi la Polisi kwa kutoa taarifa mapema kuhusu matukio au watu mnaowatilia shaka katika maeneo yenu ili kwa pamoja tuweza kulinda amani na usalama wetu," alisema Mkaguzi Mwinuka.
Mkaguzi Mwinuka alisema kuwa ataendelea kushirikiana na wadau mbalimbali kuhakikisha jamii inaendelea kuwa salama, yenye utulivu na inayo heshima sheria kwa manufaa ya jamii kiujumla.
Mwisho Mkaguzi Mwinuka alihitimisha kwa kauli isemayo "Taarifa yako ni msaada mkubwa kwa usalama wa taifa, Usikae kimya toa taarifa kwa wakati"






0 comments:
Post a Comment