Nafasi Ya Matangazo

August 31, 2025









Na Mwandishi Wetu, Mwanza
Viongozi wa klabu zinazoshiriki michezo ya 39 ya Shirikisho la Michezo ya Wizara, Idara, Wakala za Serikali na Ofisi za wakuu wa Mikoa (SHIMIWI) leo tarehe 30 Agosti, 2025 zimepanga makundi katika uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.

Viongozi hao takribali 60 walioshiriki zoezi hilo wamepanga makundi ya michezo ya mpira wa miguu, netiboli, na kuvuta kamba kwa wanaume na wanawake, ambapo michezo itaanza rasmi tarehe Mosi Septemba, 2025.

Katibu Mkuu wa SHIMIWI, Bw. Alex Temba amesema michezo hii inafanyika kwa mujibu wa kalenda ya mwaka ya shirikisho hili kunafanyika michezo hii, ambapo itafunguliwa rasmi Septemba 6 kwenye uwanja wa CCM Kirumba.

Hatahivyo, Bw. Temba amesema uongozi unatarajia ushiriki wa klabu zaidi ya 70 za wizara, Idara, wakala na ofisi za wakuu wa mikoa kwa Tanzania Bara.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kamati ya Ufundi ya michezo hiyo, Bw. Apollo Kayungi amesema makundi katika michezo hiyo yamepangwa kuanzia A hadi H, na yanaidadi ya timu nne na mengine tano.

“Upangaji wetu wa makundi ni wa wazi, kwa viongozi wa timu kuchagua karatasi yenye herufi inayomuonyesha kuwa ndio kundi lake na timu zimefanya hivyo na kutokana na wingi wa timu tumefanikiwa kupata makundi nane ikiwa ni A hadi H na ndani yake yanakuwa na timu nne nne lakini kuna nyingine zipo tano,” amesema Bw. Kayungi

Halikadhalika, Bw. Kayungi ametoa wito kwa klabu shirikishi kuhakikisha wanaingiza timu uwanjani kulingana na ratiba zao, na endapo itatokea timu kushindwa kufika uwanjani kwa sababu zao, Shirikisho litawasilisha taarifa kwa mwajiri wake.

“Pamoja na kwamba tunatawaliwa na kanuni za mashindano za kutozwa faini kikanuni na kuandikiwa barua kwa mwajiri wao ili wawajibishwe kwa ubadhirifu, lakini pia sisi tunaongozwa na kanuni, miongozo na taratibu za utumishi wa umma, hivyo tuhakikishe tunazifuata na sio kuzikiuka,” amesisitiza Bw. Apollo.
Posted by MROKI On Sunday, August 31, 2025 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo