Nafasi Ya Matangazo

August 06, 2025












Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Dkt. Janet R. Lekashingo ameongoza kikao cha Kamisheni ya Tume ya Madini kilichofanyika jijini Dodoma kwa lengo la kupokea na kujadili taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya Tume ya Madini kwa kipindi cha miezi mitatu sambamba na kuweka mikakati ya kuhakikisha Sekta ya Madini inaendelea kuwa na mchango mkubwa kwenye ukuaji wa uchumi wa nchi.

Kikao hicho  kilichoshirikisha Makamishna wa Tume na Menejimenti kimeendelea kuweka mikakati mipya ya kuhakikisha Sekta ya Madini inaendelea kuwa na mchango kwenye Pato la Taifa kupitia uboreshaji wa usimamizi kwenye shughuli za uchimbaji na biashara ya madini, ukusanyaji wa maduhuli na masoko ya madini na udhibiti wa utoroshaji wa madini. 

Mara baada ya kupokea taarifa za mafanikio kutoka kwa Katibu Mtendaji wa Tume ya Madini, Mhandisi Ramadhani Lwamo, Kamati za  Ufundi, Ushirikishwaji wa Watanzania katika Sekta ya Madini,  Fedha na Mipango na  Ajira na Usimamizi wa Rasilimaliwatu, Dkt. Janet Lekashingo amepongeza kazi nzuri inayofanywa na Tume ya Madini hasa kwenye eneo la ukusanyaji wa maduhuli, usimamizi wa masoko ya madini na vituo vya ununuzi wa madini vilivyoanzishwa nchini, kuimarika kwa usalama kwenye shughuli za uchimbaji wa madini, ushirikishwaji wa watanzania katika Sekta ya Madini na mchango wa kampuni za madini kwa Jamii.

Katika hatua nyingine, Dkt. Lekashingo amesema kuwa Tume ya Madini imeendelea kujipanga katika kuhakikisha inavuka lengo la ukusanyaji wa maduhuli kwa mwaka wa fedha 2025/2026 la shilingi Trilioni 1.2 na mchango wa Sekta ya Madini kwenye Pato la Taifa kuendelea kukua.

Kupitia kikao hicho changamoto mbalimbali katika Sekta ya Madini zimejadiliwa sambamba na kuweka mikakati mbalimbali kupitia Kamati za Ufundi, Rasilimaliwatu, Fedha na Ushirikishwaji wa Watanzania katika Sekta ya Madini lengo likiwa ni kuhakikisha wachimbaji wa madini wanafanya kazi katika mazingira ambayo ni rafiki na kujipatia kipato ili Sekta ya Madini iendelee kuwa na mchango mkubwa kwenye Pato la Taifa.
Posted by MROKI On Wednesday, August 06, 2025 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo