Nafasi Ya Matangazo

August 31, 2025









Mgombea Mwenza wa Kiti cha Urais kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) Balozi Dkt Emmanuel John Nchimbi akiwahutubia Wananchi wa Tarime mjini ikiwa ni sehemu ya muendelezo wa Kampeni zake ndani ya mkoa wa Mara.

Baada ya kuwahutubia Wananchi wa Tarime mjini,Balozi Dkt.Nchimbi akiwa ni mgombea mwenza wa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan pia alimnadi mgombea ubunge wa jimbo la  Tarime mjini, Esther Matiko,Wagombea Ubunge na Madiwani wa Mkoa huo.

Dkt.Nchimbi ambae ni Mgombea mwenza wa Dkt Samia Suluhu Hassan kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), ameanza kampeni zake mkoani Mara jana Agosti 30, 2025 akitokea mkoa wa Mwanza, ikiwa ni katika harakati za kuomba ridhaa ya Watanzania  walioko Kanda ya Ziwa katika Uchaguzi mkuu unaotarajiwa Kufanyika Oktoba 29, 2025.
Posted by MROKI On Sunday, August 31, 2025 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo