Serikali imetoa wito kwa sekta binafsi na wananchi kwa ujumla kuendelea kuchangamkia fursa za uwekezaji katika biashara ya kaboni ili kuinua uchumi na kuhifadhi mazingira kwa kupanda miti na kuitunza.
Pia, Mhe. Khamis amesistiza Serikali itaendelea kusimamia sheria, kanuni miongozo na taratibu, katika uendeshaji wa biashara hii ili wananchi wavutiwe na wanufaike na uwepo wa biashara hiyo.
Mhe. Khamis alitaja mikakati hiyo kuwa ni mbali ya kuanzisha kisheria NCMC sanjari na Kanuni za Udhibiti na Usimamizi wa Biashara ya Kaboni (2022), ambazo zimefanyiwa marekebisho mwaka 2023.
Halikadhalika, Kutoa elimu kwa umma kuhusu biashara ya kaboni imeendelea ktolewa pamoja na kuhamasisha sekta binafsi kuwekeza katika biashara hiyo zikiwemo ambazo.
Kwa upande
mwngine, Naibu Waziri Khamis alisema kutokana na uwepo wa misitu mikubwa upande
wa Zanzibar, visiwa hivyo vinakwenda kunufaika na matunda ya biashara ya
kaboni.
Alisema Ofisi ya Makamu wa Rais kushirikiana na Mamlaka ya Hifadhi ya Mazingira ya Zanzibar (ZEMA), wawikilishi, wakuu wa mikoa na wilaya pamoja na mawziri kutoa kutoa elimu kwa wananchi wa visiwa hivyo kutunza miti ili kunuifa na biashara ya kaboni.
Alisema hayo wakati akijibu swali la Mbunge wa Amani Mhe. Abdul Yussuf Maalim aliyetaka kujua kuna mkakati gani wa kuwashirikisha wadau wa Zanzibar ili waweze kunufaika na biashara ya kaboni.
Hivyo, biashara ya kaboni imeendelea kuleta manufaa kwa Serikali na kwa wananchi kwa ujumla hususan katika halmashauri zinazozunguka misitu hapa nchini kwa kujengewa miundombinu kutokana na mapato yanayotokana na biashara hiyo.
0 comments:
Post a Comment