Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amefanya uhamisho na mabadiliko ya
uteuzi wa viongozi mbalimbali. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu
Kiongozi Balozi Dkt. Moses Kusiluka, viongozi waliohamishwa na walioteuliwa ni
kama ifuatavyo:-
A: Uhamisho wa Wakuu wa Mikoa
1. Mhe. Kenan Laban Kihongosi amehamishwa kutoka Mkoa wa Simiyu kwenda kuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha; na
2. Mhe. Anamringi Macha amehamishwa kutoka Mkoa wa Shinyanga kwenda kuwa Mkuu wa Mkoa wa Simiyu.
B: Uteuzi wa Wakuu wa Mikoa
A: Uhamisho wa Wakuu wa Mikoa
1. Mhe. Kenan Laban Kihongosi amehamishwa kutoka Mkoa wa Simiyu kwenda kuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha; na
2. Mhe. Anamringi Macha amehamishwa kutoka Mkoa wa Shinyanga kwenda kuwa Mkuu wa Mkoa wa Simiyu.
B: Uteuzi wa Wakuu wa Mikoa

1. Balozi Simon Nyakoro Sirro ameteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kigoma;
2. Mhe. Kheri Denice James ameteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Iringa;
3. Mhe. Mboni Mohamed Mhita ameteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga;
4. Mhe. Beno Morris Malisa ameteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mbeya; na
5. Mhe. Jabiri Omari Makame ameteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Songwe.
1. Bi. Agnes Meena ameteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi.
D: Uhamisho wa Makatibu Tawala wa Mikoa
1. Bw. Rashid Kassim Mchata amehamishwa kutoka Mkoa wa Pwani kwenda kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga; na
2. Bi. Pili Hassan Mnyema amehamishwa kutoka Mkoa wa Tanga kwenda kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Pwani.
E: Uteuzi wa Makatibu Tawala wa Mikoa
1. Bw. Abdul Rajab Mhinte ameteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam; na
2. Dkt. Frank Hawasi ameteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Songwe.
F: Uhamisho wa Naibu Katibu Mkuu
1. Dkt. Hussein Mohamed Omar amehamishwa kutoka Wizara ya Kilimo kwenda kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia.
G: Uteuzi wa Naibu Makatibu Wakuu
1. Prof. Peter Lawrence Makenga Msoffe ameteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Makamu wa Rais anayeshughulikia masuala ya mazingira; na
2. Mhandisi Athumani Juma Kilundumya ameteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Kilimo anayeshughulikia masuala ya maendeleo ya mazao na usalama wa chakula.
H: Uhamisho wa Wakuu wa Wilaya
1. Mhe. Solomon Jonas Itunda amehamishwa kutoka Wilaya ya Songwe kwenda kuwa Mkuu wa Wilaya ya Mbeya;
2. Mhe. Japhari Kubecha Mghamba amehamishwa kutoka Wilaya ya Handeni kwenda kuwa Mkuu wa Wilaya ya Gairo; na
3. Mhe. Amir Mohamed Mkalipa amehamishwa kutoka Wilaya ya Arumeru kwenda kuwa Mkuu wa Wilaya ya Ilemela.
I: Uteuzi wa Wakuu wa Wilaya
1. Bw. Estomin Mwatuyobe Kyando ameteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kilolo;
2. Bw. Ayubu Yasin Sebabile ameteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Muheza;
3. Bi. Thecla Mkuchika ameteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Butiama;
4. Bi. Angelina Marco Lubela ameteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Serengeti;
5. Bw. Maulid Hassan Dotto ameteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Mvomero;
6. Bi. Rukia Ally Zuberi ameteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Mwanga;
7. Bw. Mwinyi Ahmed Mwinyi ameteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Arumeru;
8. Bw. Jubilete Win Lauwo ameteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Magu;
9. Bi. Mikaya Tumaini Dalmia ameteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni;
10. Bw. Thomas Mendraid Myinga ameteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Sikonge;
11. Bi. Gloriana Julius Kimath ameteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Monduli;
12. Bi. Upendo Bert Wella ameteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Tabora;
13. Bw. Denis Gervas Masanja ameteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Tunduru;
14. Bw. Fadhil Emanuel Nkurlu ameteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Songwe;
15. Bw. Benjamin Samwel Sitta ameteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Iringa;
16. Bw. Salum Nyamwese ameteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Handeni; na
17. Bw. Frank John Mkinda ameteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kahama;
J: Uteuzi wa Makatibu Tawala wa Wilaya
1. Bi. Mwanamwaya Kombo ameteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Wilaya ya Mkinga;
2. Bw. Kassim Salum Kirondomara ameteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Wilaya ya Biharamulo;
3. Bw. Thobias Abwaro ameteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Wilaya ya Babati
4. Bw. Asycritus Mumena Egaruk ameteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Wilaya ya Meatu;
5. Bi. Nyakaji Etanga Mashauri ameteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Wilaya ya Kilolo;
6. Bw. Mustapha Ayubu Kimomwe ameteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Wilaya ya Rufiji;
7. Bw. Milama Masiko ameteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Wilaya ya Serengeti
8. Bw. Mpampalika Mfaume Mpampalika ameteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Wilaya ya Mwanga;
9. Bw. Richard Jackson Mwalingo ameteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Wilaya ya Mtwara;
10. Bw. Zuberi Said Zuberi ameteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Wilaya ya Magu
11. Bi. Angela Henry Mono ameteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Wilaya ya Tanga;
12. Bi. Mamndolwa Miraj Gembe ameteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Wilaya ya Same;
13. Bi. Sabina Starlin Mwajeka ameteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Wilaya ya Momba;
14. Bw. Sosthenes Chakupanyuka ameteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Wilaya ya Kaliua; na
15. Bw. Adestino Gwelino Mwilinge ameteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Wilaya ya Mbogwe.
K: Uhamisho wa Wakurugenzi Watendaji wa Halmashauri
1. Bw. Justice Laurent Kijazi amehamishwa kutoka Halmashauri ya Manispaa ya Iringa kwenda kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Jiji la Mbeya; na
2. Bi. Zaina Mfaume Mlawa amehamishwa kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Bahi kwenda kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa.
L: Uteuzi wa Wakurugenzi Watendaji wa Halmashauri
1. Bw. Raymond Mweli ameteuliwa kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali;
2. Bi. Adelina Enock Mfikwa ameteuliwa kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Bukombe ;
3. Bw. Iddi Ally Ndabona ameteuliwa kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi;
4. Bw. Hamisi Hamidu Idd ameteuliwa kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Busega;
5. Bw. Mwarami Seif ameteuliwa kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Nzega;
6. Bi. Newaho Mkisi ameteuliwa kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Meatu;
7. Bi. Zainab Salum Mgomi ameteuliwa kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Mji wa Nanyamba;
8. Dkt. John Marco Pima ameteuliwa kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Manispaa ya Tabora;
9. Bi. Albina Willium Mtumbuka ameteuliwa kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Bahi;
10. Bw. Paulo Francis Faty ameteuliwa kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero;
11. Bw. Shabani Kabelwa ameteuliwa kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua; na
12. Bw. Vicent Augustino Mbua ameteuliwa kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe.
M: Uteuzi wa Mkuu wa Taasisi1. Mhandisi Machibya Masanja ameteuliwa kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania (TRC).
Uapisho wa Wakuu wa Mikoa, Katibu Mkuu, Makatibu Tawala wa Mikoa na Naibu Makatibu Wakuu wateule utafanyika kwa tarehe itakayopangwa baadaye.
0 comments:
Post a Comment