Kamishna Msaidizi wa Idara ya Uendelezaji wa Fedha, Wizara ya Fedha, Bi. Dionesia Mjema, akizungumza wakati akifunga mafunzo kwa Waratibu wa Biashara ya Huduma Ndogo za Fedha kutoka ngazi ya Wizara, Mikoa na Halmashauri, iliyofanyika katika Ukumbi wa Kambarage, Treasury Square, jijini Dodoma.
Kamishna Msaidizi, Idara ya Uendelezaji wa Sekta ya Fedha, Wizara ya Fedha, Bi. Dionesia Mjema, akiteta jambo na Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa SELF, Bi. Sentiel Yona, wakati wa mafunzo kwa Waratibu wa Biashara ya Huduma Ndogo za Fedha kutoka ngazi ya Wizara, Mikoa na Halmashauri, iliyofanyika katika Ukumbi wa Kambarage, Treasury Square, jijini Dodoma.
Washiriki wa mafunzo yaliyotolewa na Wizara ya Fedha kwa Waratibu wa Biashara ya Huduma Ndogo za Fedha kutoka ngazi ya Wizara, Mikoa na Halmashauri, wakibadilishana uzoefu baada ya kumalizika kwa mafunzo kwa waratibu hao yaliyofanyika katika Ukumbi wa Kambarage, Treasury Square, jijini Dodoma.
Mmoja wa watoa mada kuhusu huduma za uwekezaji, Afisa Mauzo, Watumishi Housing Investment, Bw. Jafari Chaukunde, wakati wa mafunzo kwa Waratibu wa Biashara ya Huduma Ndogo za Fedha kutoka ngazi ya Wizara, Mikoa na Halmashauri, yaliyotolewa na Wizara ya Fedha, yaliyofanyika katika Ukumbi wa Kambarage, Treasury Square, jijini Dodoma.
Kamishna Msaidizi, Idara ya Uendelezaji wa Sekta ya Fedha, Wizara ya Fedha, Bi. Dionesia Mjema (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Kamati ya maandalizi ya mafunzo kwa Waratibu wa Biashara ya Huduma Ndogo za Fedha kutoka ngazi ya Wizara, Mikoa na Halmashauri, baada ya kumalizika kwa halfa ya kufunga, iliyofanyika katika Ukumbi wa Kambarage, Treasury Square, jijini Dodoma. Kulia ni Afisa Msimamizi Fedha Mkuu, Idara ya Uendelezaji Fedha Wizara ya Fedha Bw. Magesa Mafuru na kushoto ni Afisa Maendeleo ya Jamii (TAMISEMI) Bi. Everine Kapologwe.
Kamishna Msaidizi, Idara ya Uendelezaji wa Sekta ya Fedha, Wizara ya Fedha, Bi. Dionesia Mjema (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Waratibu wa Biashara ya Huduma Ndogo za Fedha kutoka ngazi ya Wizara, Mikoa na Halmashauri, baada ya kumalizika kwa halfa ya kufunga, katika Ukumbi wa Kambarage, Treasury Square, jijini Dodoma. Kulia ni Afisa Msimamizi Fedha Mkuu, Idara ya Uendelezaji Fedha Wizara ya Fedha Bw. Magesa Mafuru na kushoto ni Afisa Maendeleo ya Jamii (TAMISEMI) Bi. Everine Kapologwe.
Kamishna Msaidizi, Idara ya Uendelezaji wa Sekta ya Fedha, Wizara ya Fedha, Bi. Dionesia Mjema (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Waratibu wa Biashara ya Huduma Ndogo za Fedha kutoka ngazi ya Wizara, Mikoa na Halmashauri, baada ya kumalizika kwa halfa ya kufunga, katika Ukumbi wa Kambarage, Treasury Square, jijini Dodoma. Kulia ni Afisa Msimamizi Fedha Mkuu, Idara ya Uendelezaji Fedha Wizara ya Fedha Bw. Magesa Mafuru na kushoto ni Afisa Maendeleo ya Jamii (TAMISEMI) Bi. Everine Kapologwe.*********************
Na. Josephine Majura na Chedaiwe Msuya, WF,
Dodoma
Katika kuhakikisha usimamizi madhubuti wa
Sekta ya Huduma Ndogo za Fedha, Serikali imewaagiza waratibu wa biashara ya
huduma ndogo za fedha kote nchini kuhakikisha wanasimamia kikamilifu
utekelezaji wa Sera na Sheria za Huduma Ndogo za Fedha katika maeneo wanayoyasimamia
ili kuwabaini na kuwachukulia hatua watoa huduma wanaotoa huduma kinyume na
utaratibu uliowekwa.
Agizo hilo limetolewa na Kamishna Msaidizi wa
Idara ya Uendelezaji wa Fedha, Wizara ya Fedha Bi. Dionesia Mjema, wakati
akifunga mafunzo ya kitaalamu kwa watoa huduma ndogo za fedha kutoka katika
ngazi za mikoa, wilaya na halmashauri, yaliyolenga kuwaongezea ujuzi wa
kiutendaji katika kutambua changamoto, kushughulikia ukiukwaji wa sheria na
kuwajengea uwezo wa kusimamia kwa ufanisi huduma hizo.
“Ni muhimu kila mmoja wetu awe mstari wa
mbele katika kuhakikisha kuwa Sheria ya Huduma Ndogo za Fedha inatekelezwa
ipasavyo, na wale wanaokiuka Sheria hiyo wanachukuliwa hatua stahiki,” alisema
Bi. Mjema.
Alisisitiza kuwa utekelezaji wa Sheria si
chaguo bali ni wajibu wa kila mtoa huduma na msimamizi wa sekta hii, kwa kuwa
utekelezaji huo ndio msingi wa kuhakikisha uwajibikaji, uadilifu, na uendelevu
wa huduma ndogo za fedha katika kuwawezesha wananchi kiuchumi.
Aidha, aliwasisitiza kujenga mazoea ya kuandaa
na kuwasilisha taarifa za utekelezaji wa Sheria hizo kila baada ya miezi
mitatu, kwa mujibu wa miongozo, kwa kuwa taarifa hizo ni nyenzo muhimu katika
kutathmini maendeleo, changamoto na mafanikio ya utekelezaji wa sheria katika
maeneo mbalimbali ya nchi.
Bi. Mjema, aliwasihi waratibu hao
kushirikiana kwa karibu na maafisa ushirika, wahamasishaji, wasajili, pamoja na
maafisa maendeleo ya jamii, ili kuhakikisha kuwa utekelezaji wa Sera na Sheria
za Huduma Ndogo za Fedha unafanyika kwa ufanisi.
“Ushirikiano huo unatarajiwa kujenga mfumo
madhubuti na endelevu wa huduma ndogo za fedha, unaolenga kuwafikia wananchi wa
kipato cha chini kwa kutumia mbinu bora, salama na zenye ufanisi, ili kuchochea
ustawi wa kiuchumi na kuchangia maendeleo jumuishi ya taifa zima”alisema Bi.
Mjema.
Kwa upande wake, Mratibu wa Biashara ya
Huduma Ndogo za Fedha mkoani Mbeya, Bi. Sebastiana Mwapinga, ambaye alikuwa
miongoni mwa washiriki wa mafunzo hayo, alisema kuwa mafunzo hayo yamekuwa
kichocheo muhimu cha mabadiliko chanya, na kwamba wataendelea kuboresha
utendaji wao hususan katika maeneo yaliyokuwa na changamoto hapo awali, ili
kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora za kifedha zitakazowawezesha kuinua
hali zao za kiuchumi.
Naye, mmoja wa wahamasishaji, Bi. Teodomila Mwenda,
amesema kuwa hatua ya Serikali kuwapatia mafunzo na kuwajengea uwezo wa
kitaalamu siyo tu imedhihirisha dhamira yake ya dhati ya kuimarisha sekta hiyo,
bali pia imeongeza ari na motisha kwao kuendelea kutoa elimu kwa ufanisi zaidi.
Katika mafunzo hayo ya siku mbili
yaliyoandaliwa na Wizara ya Fedha, taasisi mbalimbali zilipata fursa ya kutoa
elimu kuhusu huduma za uwekezaji wanazotoa ikiwemo Kampuni ya Uwekezaji UTT-
AMIS, Mfuko wa SELF pamoja Watumishi Housing Investment ambazo ni muhimu kwa
wananchi kuzifahamu na kuzitumia ipasavyo ili kuongeza kipato chao na kuboresha
maisha yao ya kiuchumi.
Jumla ya waratibu 130 wa huduma ndogo za
fedha kutoka ngazi ya Wizara, Mikoa na Halmashauri wamepatiwa mafunzo ya
kitaalamu katika maeneo mbalimbali, yaliyolenga kuwaimarisha katika kusimamia
na kufuatilia kwa ufanisi utoaji wa huduma ndogo za fedha katika ngazi za watoa
huduma.
0 comments:
Post a Comment