Naibu Waziri wa Madini Dkt. Steven Kiruswa amesema kuwa, maendeleo ya Sekta ya Madini yanapelekea kuwa kitovu cha uchumi nchini, hii ni kutokana na mageuzi mbalimbali yanayoendelea kufanyika.
Dkt. Kiruswa ameyasema hayo leo Juni 13, 2025, wakati akizungumza na vyombo vya habari mapema baada ya kutembelea mabanda katika maonesho ya madini yanayoendelea kufanyika wilayani Ruangwa.
Akielezea kuhusu uwekezaji wa ndani Dkt. Kiruswa ameeleza kuwa, Tanzania imekuwa kivutio kikubwa cha wawekezaji katika Sekta ya Madini kutokana na utajiri wake wa madini mbalimbali yakiwemo madini ya kinywe, makaa ya mawe pamoja na madini adimu na madini mkakati.
Kuhusu kukua kwa Sekta ya Madini, Dkt. Kiruswa amebainisha kuwa, Sekta hii imeendelea kukua kwa kasi ambapo kwa sasa inachangia asilimia 10.1 kwenye Pato la Taifa.
Dkt. Kiruswa ameongeza kuwa, ukuaji huu unatokana na mipango endelevu hususan katika uongezaji thamani madini, uwekezaji wa mitaji ya ndani na ya nje pamoja na Sera madhubuti za usimamizi wa rasilimali madini nchini.
Pamoja na mambo mengine, Serikali imeendelea kusisitiza kuhusu uongezaji thamani madini kufanyika ndani ya nchi kabla ya kusafirishwa nje ya nchi, ujenzi wa viwanda vya kusafisha dhahabu, ujenzi wa maabara za uchenjuaji na uchakataji madini.
*# MineralValueAddition*
*#GDP:10.1%FromMineralSector*
*#Vision2030:MadiniNiMaishaNaUtajiri*
0 comments:
Post a Comment