Nafasi Ya Matangazo

June 14, 2025

 
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deus Sangu akizungumza na baadhi ya wananchi, watumishi na baadhi ya viongozi kutoka Taasisi mbalimbali wakati akizindua Jengo la TAKUKURU  Wilaya ya Nzega Mkoani Tabora ambalo limegharimu kiasi cha Sh. Mil. 314.2 hadi kukamilika kwake.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deus Sangu akiwa na baadhi ya viongozi akikata utepe wakati akizindua Jengo la TAKUKURU  Wilaya ya Nzega Mkoani Tabora ambalo limegharimu kiasi cha Sh. Mil. 314.2 hadi kukamilika kwake.
Mkuu wa wilaya ya Nzega, Mhe. Naitapwaki Tukai akizungumza kabla ya kumkaribisha  Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deus Sangu  kwa ajili ya kuzindua Jengo la TAKUKURU  Wilaya ya Nzega Mkoani Tabora ambalo limegharimu kiasi cha Sh. Mil. 314.2 hadi kukamilika kwake.
Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU, Bw. Crispin Chalamila akizungumza kabla ya kumkaribisha  Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deus Sangu  kwa ajili ya kuzindua Jengo la TAKUKURU  Wilaya ya Nzega Mkoani Tabora ambalo limegharimu kiasi cha Sh. Mil. 314.2 hadi kukamilika kwake.
**********
Na. Lusungu Helela- NZEGA  
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deus Sangu amesema Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) imejidhatiti kuhakikisha inadhibiti vitendo vya rushwa kabla, wakati na hata baada ya Uchaguzi Mkuu huku akiwaasa wagombea kujiepusha na vitendo vya rushwa huko majimboni kwani TAKUKURU ipo kazini.

Amesema kitendo cha  Rais Mhe.Dkt.Samia Suluhu Hassan kutoa jumla ya magari mapya  195 kwa ajili ya  TAKUKURU ni uthibitisho tosha kuwa anachukia vitendo vya rushwa.

Mhe.Sangu ametoa kauli hiyo leo  wakati akizindua Jengo la TAKUKURU  Wilaya ya Nzega Mkoani Tabora ambalo limegharimu kiasi cha Sh. Mil. 314.2 hadi kukamilika kwake.

Amesema TAKUKURU  itawakamata wale wote watakaothubutu kutoa rushwa ya aina yeyote ile kwa lengo la kuwarubuni wapiga kura "Msikubali kurubuniwa na rushwa na atakayethubutu kufanya hivyo  toeni taarifa kwa TAKUKURU" amesisitiza Mhe.Sangu

Amesema mbali ya kutoa magari hayo, katika kipindi chake cha uongozi Rais.Mhe.Dkt.Samia Suluhu Hassan ametoa fedha za kujenga jumla  ofisi  25 katika mikoa na wilaya mbalimbali nchini kwa lengo la kuwawezesha watumishi wa TAKUKURU  kufanya kazi katika mazingira rafiki hususan katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi Mkuu

Aidha, Mhe, Sangu amemshukuru Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa uwekezaji mkubwa alioufanya kwa taasisi hiyo ambapo katika kipindi chake cha uongozi ameajiri watumishi wapya  1900 ikiwa ni nusu ya watumishi aliowakuta

Akizungumzia madhara ya kuchagua viongozi kwa njia ya rushwa, Mhe, Sangu amesema vitendo vya rushwa na makosa mengine yanayofanyika wakati wa uchaguzi huwapoka  wapiga kura haki ya kumchagua  mgombea wanayemtaka.

Ameongeza kuwa vitendo hivyo vya rushwa huwanyima haki baadhi ya wagombea kushiriki na kushindana kwa usawa katika uchaguzi.

Naye Mkuu wa wilaya ya Nzega, Mhe. Naitapwaki Tukai amesema yeye kama Mwakilishi wa Rais katika  wilaya hiyo kwa kushirikiana na Ofisi ya TAKUKURU wamejidhatiti kuhakikisha hakuna mtu yeyote atakayechaguliwa kuwa Kiongozi katika wilaya hiyo kwa njia ya rushwa.

" Mtu yeyote mwenye nia kugombea katika uchaguzi Mkuu kwa njia ya rushwa,   hana nafasi katika wilaya hii amesisitiza Mhe, Tukai

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU, Bw. Crispin Chalamila amesema TAKUKURU imewezeshwa vitendea kazi hivyo jukumu walilonalo kwa sasa ni kufanya kazi kwa maslahi ya taifa kabla, baada na hata baada ya Uchaguzi Mkuu. 
Posted by MROKI On Saturday, June 14, 2025 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo