Nafasi Ya Matangazo

June 30, 2025

Meneja Benki ya CRDB Kanda ya Ziwa, Lusingi Sitta (pichani) amechukua fomu ya kuomba ridhaa ya kugombea ubunge katika Jimbo la Kisesa lililopo Wilaya ya Meatu mkoani Simiyu.

Hatua hiyo inaongeza joto la uchaguzi ndani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) katika Jimbo hilo ambalo kwa sasa mbunge wake ni Luhaga Mpina.

Sitta ameweka wazi maono na ahadi zake kwa wana Kisesa ikiwa atapata ridhaa ya kuwa mbunge wao kuwa ni pamoja na;

Kutahakikisha Kisesa inapata maji safi kupitia visima na miradi ya maji ya kudumu.

Pia kupigania bajeti ya kujenga au kuboresha shule na zahanati vijijini.

"Nitahamasisha vijana kujiunga na vikundi vya uzalishaji na nitawatafutia mitaji na mafunzo" amesisitiza Sitta.

Ameongeza kuwa atafanya kazi vyema na Serikali ili kuhakikisha barabara kuu na za vijijini zinajengwa au kukarabatiwa ili zipitika wakati wote.
Posted by MROKI On Monday, June 30, 2025 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo