Mbunge wa Jimbo la Kondoa na Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji, amechukua na kurejesha fomu ya kuomba ridhaa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) na wananchi ili kuwania tena nafasi ya Ubunge wa Jimbo hilo katika uchaguzi mkuu ujao.
Dkt. Ashatu ameichukua na kuirejesha fomu hiyo leo tarehe 29 Juni, 2025 katika Ofisi za CCM Wilaya ya Kondoa mkoani Dodoma mbele ya Kaimu Katibu wa CCM Wilaya ya Kondoa, Ndg. Jumaa Seif.
Akizungumza mara baada ya kurejesha fomu hiyo, Dkt. Ashatu ameeleza nia yake kuu ya kutaka kugombea tena nafasi hiyo ili kukamilisha mafanikio yaliyopatikana katika kipindi cha uongozi wake, hususan katika sekta ya elimu.
Baadhi ya mafanikio hayo ni pamoja na sekta muhimu za elimu, maji, nishati ya umeme na miundombinu ya barabara hususani madaraja makubwa yaliyoshindikana kwa muda mrefu.
0 comments:
Post a Comment