Nafasi Ya Matangazo

May 08, 2025

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Mhe. Ridhiwani Jakaya Kikwete amekutana na kufanya mazungumzo na viongozi wa Benki ya NMB wakiongozwa na Meneja Mahusiano Benki na Serikali Bi. Vicky Bishubo.
 
Ziara hiyo ya viongozi hao wa NMB pamoja na mambo mengine ilikua na lengo la utambulisho wa watendaji hao kwa Waziri Kikwete.
 
Waziri Kikwete alishukuru kwa ujio wao na kuwatambulisha katika maeneo ambayo Benki ya NMB inaweza kushirikiana na Serikali hususani katika Wizara hiyo ya , waliokuja kujitambulisha na kunitambulisha bidhaa mbalimbali zinazotolewa na Benki hiyo.
 
Katika kikao hicho niliwakaribisha ofisini kwetu na kuwatambulisha baadhi ya maeneo ambayo benki hiyo inaweza shirikiana na Serikali katika kufanikisha uwezeshaji Vijana na Jamii.


Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Mhe. Ridhiwani Jakaya Kikwete akifafanua jambo kwa watendaji hao wa Benki ya NMB.

Meneja Mahusiano Benki na Serikali Bi. Vicky Bishubo akifafanua jambo.

Posted by MROKI On Thursday, May 08, 2025 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo