Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Ndg.Ridhiwani Jakaya Kikwete leo amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa China nchini Tanzania, Chen Mingjian.
Wawili hao wamekutana Dodoma ambapo Balozi huyo alimtembelea Waziri Kikwete kwa lengo la kujitambulisha.
"Nimekutana na kufanya mazungumzo na ujumbe wa Ubalozi wa Jamhuri ya Watu wa China ukiongozwa na Balozi wa China Nchini Balozi Ofisini, Dodoma," amesema Kikwete.
Balozi Mingjian alisema lengo la ziara hiyo ni kuendelea kuimarisha mahusiano ya Kidiplomasia baina ya nchi hizo mbili za China na Tanzania.
Aidha, Balozi huyo na ujumbe wake walikumbusha maeneo muhimu ya ushirikiano haswa katika mafunzo ya kujenga ujuzi na ufundi huku msisitizo mkubwa ukiwa kuwaandaa vijana watakaopambana na mabadiliko makubwa ya kidunia hasa katika mapinduzi ya Teknolojia.
Nae Waziri Kikwete kwa upande wake aewakikishia kuwa Tanzania itaendelea kuenzi uhusiano uliopo baina ya nchi z na kuwa tutaendeleza uhusiano huu kwa kuimarisha maeneo yote ambayo yanatukutanisha katika mashirikiano haya.
Pia ameishukuru serikali ya China kwa mabadiliko makubwa ambayo yanaelekea kukuza ujuzi kwa vijana wa Kitanzania na nia yao ya kufanya maonyesho makubwa ya Kazi yanayolenga kufunua fursa za vijana wa kitanzania kujiajiri na kufungua milango ya kuajiriwa na makampuni makubwa ya kigeni yakiwemo ya China nchini hapa.
0 comments:
Post a Comment