Nafasi Ya Matangazo

May 01, 2025


Na Mwandishi Wetu, Singida
Watumishi wa umma waliokuwa wakishiriki kwenye michezo ya Kombe la Mei Mosi mkoani Singida, wamechangia mahitaji muhimu ya kibinadamu yenye thamani ya kiasi cha Tshs. Mil. 14,492,000 na kupeleka kwenye vituo sita vya wahitaji.

Mwenyekiti wa Kamati ya michuano ya Mei Mosi, Bi. Roselyne Massam amesema huu ni utaratibu waliojiwekea kwa kila mwaka katika mkoa ambao wanaendesha michuano hiyo, kutoa kwa jamii yenye uhitaji kwa watumishi kujichangisha wenyewenye kutoka mifukoni mwao na kununua mahitaji muhimu kwa binadamu.

Bi. Massam amesema kwa mwaka huu wameweza kutembelea vituo sita vyenye watoto wenye uhitaji wenye umri wa kuanzia miaka mitatu hadi 15 vya mkoani hapa.

“Tumetembelea vituo vya Safina, Amani, Upendo, Dhinurey, Malaika wa Matumaini na Ipembe shule ya Msingi, ambapotumepeleka mahitaji ya vyakula kama mchele, maharage, sukari, mafuta kula, juisi, chumvi, miswaki, dawa za meno, mabegi ya shule, viatu vya kushindia, taulo za kike, mafuta ya kujipaka, magodoro, mashuka, neti, sabuni za unga na vipande,” amesema Bi. Massam.

Hatahivyo, ametoa wito kwa jamii kutoa misaada kwa wahitaji kwani walezi wao hawawezi pekee yao kukamilisha mahitaji yao, ambapo vituo vinawatoto wadogo kuanzia 62 hadi 105, ambao wengi wao ni yatima na wengine wamechukuliwa kutoka kwenye mazingira magumu ikiwemo waliookotwa baada ya kutelekezwa na wazazi wao.  
 
Naye Afisa Ustawi  Bi. Doresta Severine ameshukuru kwa misaada hii ambapo amesema kwa manispaa ya Singida inavituo vitano vyenye watoto wenye uhitaji vyenye kumilikiwa na mashirika ya kidini na watu binafsi.

“Serikali ipo karibu na vituo hivi ambavyo kwa kiasi kikubwa vinapata misaada kutoka kwa watu binafsi na taasisi za dini wanahamasisha waamini wao, lakini bado watu hawana mwamko wa kusaidia wahitaji,” amesema Bi. Doresta.

Hatahivyo, amewashukuru wanamichezo kwa kusaidia vituo vyote vitano kwa kuguswa na kupeleka mahitaji muhimu, na ameomba watu wengine wajitokeze kutoa misaada maana wahitaji hawa hawakupenda kuwepo kwenye vituo hivyo bali wamepata changamoto za kimaisha kutokana na wazazi wao wengine kufariki na wengine kuishi katika mazingira magumu.

Mtawa wa Shirika la Moyo Mtakatifu wa Yesu na Maria, ambaye pia ni msimamizi wa watoto wa kituo cha Malaika wa Matumaini, Sr. Rozalia Nicodemos amewashukuru watumishi hao kwa msaada huo mkubwa katika kituo hicho chenye watoto 62 wakiwemo wa kiume 32 na wasichana 30, ambao mahitaji yao makubwa ni vyakula vya aina mbalimbali.

“Tunashukuru sana tena mno kwa msaada huu mmetusaidia pakubwa sana katika mahitaji yote mliyoleta hasa chakula maana watoto wetu lazima wale na sisi hatuna mahali tunapopata zaidi ya misaada kama hii, na hata mmetusaidia mabegi ya watoto sasa watabeba vizuri madaftari yao kwani awali walikuwa wakibeba tu mkononi,” ameshukuru Mtawa Rozalia.

Kwa upande wake Mkuu katika kituo cha Dhinurein kilichopo kata ya Mandewe amesema kituo hicho kinawatoto 105 wakiwemo wa kike na kiume, amewashukuru wanamichezo wa Mei Mosi kwa msaada huu mkubwa wa vyakula, ambavyo ndio hitaji lao kuu kutokana na kituo kuwa na watoto wengi.

Ametoa wito kwa jamii yote kuendelea kujitoa na kusaidia watoto wenye uhitaji, maana kupitia sadaka hizi zinazotolewa zinakuwa msaada kwao na baadae wanaweza kuja  kuwasaidia watoto wengine wakiwemo wa waliotoa misaada hii.








Posted by MROKI On Thursday, May 01, 2025 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo