Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi wa
viongozi mbalimbali. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi
Balozi Dkt. Moses Kusiluka, uteuzi huo ni kama ifuatavyo:-
Arch Dkt. Fatma Kassim Mohamed ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi
ya Baraza la Taifa la Ujenzi (NCC) kwa kipindi cha pili;
Balozi Dkt. Jilly Elibariki Maleko ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Kituo cha
Kimataifa cha Mikutano cha Arusha (AICC). Balozi
Maleko anachukua nafasi ya Balozi Begum Karim Taj ambaye amemaliza muda
wake;
Prof. Eliakimu Mnkondo Zahabu ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi
ya Kituo cha Taifa cha Ufuatiliaji wa Kaboni (National Carbon
Monitoring Center – NCMC); na
Bw. Lucas Abrahamani Mwino ameteuliwa kuwa
Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA). Bw. Mwino anachukua nafasi ya Dkt. John Kedi
Mduma ambaye amemaliza muda wake.Balozi Dkt. Jilly Elibariki Malek
0 comments:
Post a Comment