Watanzania wametakiwa kumuombea kheri Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.Samia Suluhu Hassan owani kufanya hivyo ni moja ya uzalendo kwa nchi na viongozi wao.
Hayo yamesemwa na Mbunge wa Chalinze na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mh. Ridhiwani Kikwete wakati akiwahotubia Wananchi waliojitokeza kuomba dua kuiombea Nchi na Dr. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nyumbani kwake Msoga, Chalinze.
Akizungumza na umma wa Watanzania waliojitokeza kwenye dua hiyo, Mh. Kikwete amewashukuru kwa kujitokeza na kumuombea dua Mh. Rais. “ ukimuombea Rais Samia, umeiombea Tanzania, kutokana na umuhimu wa nafasi yake na yeye akiwa ndiyo mshika maono ya Nchi”. Mh. Kikwete alitumia nafasi hiyo pia kuishukuru serikali ya awamu ya 6 kwa mafanikio makubwa yaliyopatikana katika kipindi cha miaka hii ya Rais Samia Suluhu Hassan ambapo Elimu,Afya, Miundombinu n.k na kutumia nafasi hiyo pia kuwaomba wanachalinze waendelee kumuamini na kumchagua tena kwa kura nyingi.
Wakizungumza baadhi ya masheikh waliohudhuria shughuli hii, wamepokea maombi ya Mbunge wao kwa furaha na hivyo watatekeleza kwa ari kubwa.
Dua na Futari ni utaratibu ambao Mbunge wa jimbo la Chalinze amekuwa anafanya kila mwaka kipindi hiki cha Mfungo.
0 comments:
Post a Comment