Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amekutana na kufanya mazungumzo na Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Climate Investment Funds (CIF) Bi. Tariye Gbadegesin Mjini Bridgetown, Barbados.
Mazungumzo hayo yamefanyika leo Machi 14, 2025 kando ya Mkutano wa Kimataifa wa kuhusu upatikanaji wa Nishati endelevu kwa wote (Energy ForAll)
Dkt. Biteko amesema kuwa, Wizara ya Nishati iko tayari kukuza ushirikiano na Taasisi hiyo ili kuunganisha juhudi za pamoja kuhakikisha matumizi ya nishati safi ya kupikia hususan maeneo ya Vijijini.
0 comments:
Post a Comment