Bunge Bonanza la mashabiki wa Simba na Yanga wa Mjengoni (Bunge) kufanyika Februari Mosi 2025, viwanja vya John Merlin Sekondari Jijini Dodoma
Taarifa hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa Bunge Bonanza, Mheshimiwa Festo Sanga wakati Akizungumza na waandishi wa habari katika Ofisi Ndogo ya Bunge iliyopo Jijini Dar es salaam leo tarehe 24 Januari 2025
Alisema Maandalizi ya Bonanza hili linalodhaminiwa na Azania Bank lishakamilika kwa asilimia Mia moja
"Bonanza hilo linahusisha michezo yote ikiwemo Mpira wa Miguu, mpira wa pete, kuvuta kamba na michezo mingine tu" Alisema
Mhe. Festo alisema kwamba Mgeni Rasmi ambaye amependekezwa na Mheshimiwa Spika ni Ndugu Wallace Karia ambaye ni Rais wa TFF ambapo atakuwa na viongozi wengine wa bunge akiwemo Spika wa bunge Mhe. Tulia Ackson, Waziri mkuu Mhe. Kassim Majaliwa, mawaziri, manaibu mawaziri na viongozi wengine wengi
Mhe. Festo Sanga amesema lengo la Mhe. Spika kuleta bonanza hili linalohusisha mashabiki wa timu kubwa wa Yanga na Simba ni kumuunga mkono Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan katika juhudi za kupambania maendeleo ya michezo Tanzania, Malengo mengine ni kuendeleza mahusiano yaliyopo kati ya bunge na taasisi nyingine za kiserikali na taasisi nyingine binafsi lakini pia kujenga afya za kimwili ili kukabiliana na magonjwa yasiyoambukiza ambayo kila siku yanaibuka,
Nae Rais wa TFF ndugu Wallace Karia amesema amefurahishwa na mualiko huo na kwamba atashiriki kwa kiwango cha juu sana kuanzia kwenye maandalizi mpaka mwisho wa bonanza hilo, "Wito wangu kwa wana habari ni kuhakikisha mnasambaza hii taarifa ya bunge bonanza ambapo itashirikisha timu zetu pendwa ili kuwafikia wananchi wengi wapate kuhudhuria" Wallace Karia
0 comments:
Post a Comment