Nafasi Ya Matangazo

January 27, 2025

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amefungua mkutano wa Kimataifa wa Nishati unaowakutanisha Viongozi mbalimbali wa Afrika, Mashirika ya Kimataifa; Viongozi wa Benki ya Dunia, Benki ya Maendeleo ya Afrika na taasisi ya Rockefeller (M300)  inayofanyika leo Januari 27, 2025 jijini Dar es salaam. 

Mkutano huo unaandaliwa kwa pamoja baina ya Serikali ya Tanzania, Benki ya Dunia na Benki ya Maendeleo ya Afrika unawakutanisha pamoja Marais wa Nchi za Afrika 24; wawakilishi wa Wakuu wa Nchi na Serikali za Afrika 21; Wakuu wa Taasisi za Kimataifa sita (6) wakiwemo Rais wa Benki ya Dunia, Rais wa Benki ya Afrika na Rais wa Taasisi ya Rockefeller; na Washirika wa Maendeleo watano (5) watashiriki Mkutano huo. Aidha, jumla ya washiriki wengine 2,600 wa ndani na nje ya Tanzania wamejisajili kwa ajili ya Mkutano huo.












Posted by MROKI On Monday, January 27, 2025 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo