Wizara
ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki inapenda kuutaarifu umma
kwamba ziara ya kitaifa ya Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania iliyopangwa kufanyika tarehe 6 hadi 8 Novemba, 2024 nchini
Cuba imeahirishwa.
Ziara
hiyo imeahirishwa kufuatia taarifa rasmi iliyowasilishwa na Serikali ya Cuba ikitaarifu kuwa Cuba ingekumbwa na Kimbunga Rafael kuanzia tarehe 6 hadi 7
Novemba, 2024. Hali hiyo imepelekea Serikali ya Cuba kuchukua tahadhari ikiwemo
kusitisha safari zote za ndege kuingia na kuondoka Cuba.
Pamoja na kuahirishwa kwa ziara hiyo, Mhe. Rais ameelekeza shughuli zote zilizopangwa kufanyika kipindi cha ziara yake ziendelee kuratibiwa chini ya Mhe. Mahmoud Thabit Kombo (Mb), Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki akishirikiana na Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro (Mb.) Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo.
Ziara nyingine ya Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan nchini Cuba itapangwa siku za usoni baada ya nchi hizo mbili kukubaliana wakati sahihi wa ziara hiyo
0 comments:
Post a Comment