Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki anayeshughulikia masuala ya Afrika Mashariki, Mhe. Dennis Londo akikaribishwa na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa shirikisho la Urusi, Mhe. Bogdanov Mikhail Leonidovich alipowasili kwa mazungumzo yaliyofanyika pembezoni mwa Mkutano wa Kwanza wa Mawaziri wa Mambo ya Nje kutoka nchi za Afrika na Shirikisho la Urusi unaofanyika tarehe 9 hadi 10 Novemba, 2024 mjini Sochi, Urusi Naibu Waziri wa Mambo ya Nje
na Ushirikiano wa Afrika Mashariki anayeshughulikia masuala ya Afrika
Mashariki, Mhe. Dennis Londo amezinadi fursa za mbalimbali za kiuchumi ikiwemo
uwekezaji, biashara na utalii nchini Urusi wakati alipokutana kwa mazungumzo na
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa shirikisho la Urusi, Mhe. Bogdanov Mikhail
Leonidovich.
Mazungumzo ya viongozi hao
yamefanyika tarehe 10 Novemba, 2024 pembezoni mwa Mkutano wa Kwanza wa Mawaziri wa Mambo ya Nje kutoka nchi za Afrika na Shirikisho la Urusi
unaofanyika tarehe 9 hadi 10 Novemba, 2024 mjini Sochi, Urusi
Pamoja na mauala mengine,
wamejadili kuhusu Ushirikiano wa kihistoria uliopo kati ya Tanzania na Urusi
tangu enzi za Baba wa Taifa Hayati, Mwl. Julius Kambarage Nyerere na kuhaidi kuendelea kuimarisha Ushirikiano huo kati ya
nchi hizi mbili.
Aidha, kwa upande wake Mhe.
Londo ameihakikishai Serikali ya Urusi kuwa Tanzania ina nia ya dhati ya
kuhakikisha ushirikiano katika sekta za Utalii, Uwekezaji, Biashara, Kilimo,
Afya, Viwanda una imarika na kukua kwa maendeleo endelevu ya watu wake na
mataifa hayo kwa ujumla.
Vilevile, Mhe. Naibu Waziri
Londo ameeleza kuhusu uwepo wa mazingira rafiki ya uwekezaji, fursa mbalimbali
za uwekezaji zinazopatikana nchini na maeneo ya kimkakati ambayo Urusi inaweza
kushirikiana na Tanzania ili kuleta tija katika ushirikiano wake. Kadhalika,
ametoa rai kwa wawekezaji na wafanyabiashara kutoka Urusi kuchangamkia fursa
nyingi za uwekezaji na masoko zinazopatikana nchini.
Naye, Mhe. Leonidovich ameishukuru
Serikali ya Tanzania kwa kuendelea kukuza ushirikiano na Urusi na kuahidi kuwa
Urusi imejizatiti kuhakikisha ushirikiano wake na Tanzania unakuwa wenye
manufaa makubwa kiuchumi na kidiplomasi kwa pande zote.
Posted by MROKI
On Monday, November 11, 2024
No comments
0 comments:
Post a Comment