Nafasi Ya Matangazo

October 23, 2024






Na Mwandishi Maalum, Singapore
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko, amesema kuwa Tanzania inayo nafasi kubwa ya kujifunza Teknolojia ya uwambaji wa magari (Assembling) yanayotumia umeme kutoka kiwanda cha magari cha HYUNDAI kwani ni rafiki kwa mazingira na hupunguza uchafuzi wa hali ya hewa.

Dkt. Biteko ameyasema hayo leo Oktoba 23, 2024 nchini Singapore mara baada ya kutembelea kiwanda hicho ikiwa ni ziara mojawapo kwenye mkutano wa Wiki ya Nishati nchini Singapore na kusema kuwa Teknolojia kama hizi zina mchango mkubwa kwenye kuinua uchumi wa nchi na kuongeza pato la Taifa.

‘’Nawapongeza sana wenzetu hasa kwa Teknolojia na ubunifu wa haya magari pamoja na Teknolojia ya Kilimo janja (smart farm) ambapo kwanza inatumia nafasi ndogo lakini matokeo yake ni makubwa sana,’’ Amesema Dkt. Biteko.

Kuhusu Teknolojia ya kilimo janja ambacho kinaendeshwa na kampuni ya ubunifu ya HYUNDAI kwa kutumia Teknolojia mnemba (Robot) Dkt. Biteko amesema, uwepo wa Teknolojia kama hii unaongeza tija na imepunguza gharama kwenye uendeshaji wake.

Naye, Makamu wa rais na Mkuu wa Biashara na mipango kutoka HYUNDAI Motor Group amesema mafanikio hayo yanayokana na kutumia fursa iliyopo wakati wa changamoto zilizokuwepo awali kama ya matumizi ya mafuta kwenye magari ambapo haikuwa rafiki kwa mazingira pamoja na uhaba wa maeneo kwa ajili ya kilimo nchini Singapore.

Mwisho.
Posted by MROKI On Wednesday, October 23, 2024 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo