Nafasi Ya Matangazo

October 22, 2024

Watu nane wamefariki dunia na wengine 36 wamejeruhiwa baada ya mabasi mawili ya abiria kugongana uso kwa uso Mkoani Mwanza.

Mabasi hayo yaliyohusika katika ajali hiyo ni Basi la Nyehunge  na lile la Asante Rabi ambayo yaligongana  leo Oktoba 22, 2024 majira ya saa 12 asubuhi katika eneo la Ukiriguru Wilaya ya Misungwi mkoani Mwanza.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Wilbroad Mutafungwa amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kusema chanzo chake ni mwendokasi.

Amesema ajali hiyo imetokea baada ya basi la Asante Rabi lenye namba za usajili T458 DYD lilokuwa likitokea Mwanza kuelekea Jijini Arusha kujaribu kulipita gari jingine bila kuchukua tahadhari na hivyo kuligonga basi la Nyehunge.
Posted by MROKI On Tuesday, October 22, 2024 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo