Nafasi Ya Matangazo

October 19, 2024








Waziri wa Madini Mhe. Anthony Mavunde ameeleza kuhusu umuhimu wa Madini Bonanza na kueleza kuwa limelenga kuimarisha umoja, mshikamano na ushirikiano baina ya  Watumishi wa Wizara na Taasisi zake ili kuifanya Wizara kuwa familia moja.

Amesema hayo leo Oktoba 19, 2024 katika Viwanja vya Shule ya Sekondari John Merlin – Miyuji jijini Dodoma, wakati akizungumza katika Madini Bonanza lililowajumuisha Watumishi wa Wizara ya Madini na Taasisi zake. 

" Ninawapongeza kwa bonanza hili kwasababu linatusaidia kukaa  pamoja, kufurahi na kufahamiana zaidi," amesema.

Aidha, amewasisitiza watumishi  kujenga utamaduni  wa kufanya mazoezi ili kuimarisha afya zao, na kuongeza," kama mnavyofahamu hivi sasa takwimu  zinaonesha kuna changamoto kubwa ya magonjwa yasiyoambukiza hivyo kuna umuhimu mkubwa wa kufanya mazoezi,".

Katika hatua nyingine, Mhe. Mavunde amewahamasisha watumishi wa Wizara kujishiriki katika zoezi linaloendelea hivi sasa la kujiandikisha kwa ajili ya uchaguzi wa Viongozi wa Serikali za Mitaa unaotarajia kufanyika mwezi Novemba mwaka huu.

Kwa upande wake, Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Madini Terence Ngole ameeleza kuhusu  mashindano ya michezo mbalimbali yaliyofanyika yakihusisha mpira ya miguu, pete, kamba, mbio za mita 100 na mita 400 ambapo  washindi mbalimbali wamepatikana kutoka Wizara na Taasisi zake huku Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania ( GST)  ikiondoka na medali  lukuki na makombe.
Posted by MROKI On Saturday, October 19, 2024 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo