Na. Mwandishi
Wetu, Msalala
Waziri wa
Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Deogratius Ndejembi amesema baada ya
kutembelea shule ya sekondari Ntobo hakuna kasoro waliyoibaini katika ujenzi
huu wa Shule hiyo iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Msalala, huku akipongeza
zaidi kwa kubakia na salio la zaidi ya Milioni 10.
Mhe. Ndejembi
amesema haya leo Oktoba 6, 2024 alipofika shuleni hapo kutembelea na kukagua
utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika Halmashauri ya Wilaya ya Msalala
ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya siku mbili mkoani Shinyanga.
"Nawapongeza
sana Halmashauri ya Wilaya ya Msalala kwa usimamizi mzuri wa ujenzi wa shule
hii ya Ntobo, tumetembelea, tumekagua lakini mpaka sasa hakuna kasoro
tuliyoiona katika utekelezaji wa mradi huu zaidi ya yote shule inao ubora
unaoendana na thamani ya pesa na kwamba mmebakiwa na pesa zaidi ya Mil. 10 huu
ni mfano wa kuigwa," amesema Mhe. Ndejembi.
Akisoma
taarifa mbele ya mgeni rasmi, Mkuu wa Shule ya Ntobo Sekondari Mwl. Hussein
Mbwambo amesema kuwa wanayo furaha kumtaarifu Waziri kuwa ujenzi wa vyumba vya
madarasa 7, matundu 8 ya vyoo, ofisi 1 ya walimu umekamilika vizuri na kubakiwa
na salio la zaidi ya Sh. Milioni 10 ambapo wamemuomba Mkurugenzi wa Halmashauri
ya Wilaya ya Msalala awaruhusu zitumike kukarabati jengo la utawala.
Kwa upande
wake Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Macha amemshukuru Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu
Hassan kwa kuendelea kuipatia fedha za miradi ya maendeleo katika Wilaya hiyo
ambapo katika Sekta ya Elimu zimeboresha miundombinu yote muhimu ya watu wenye
ulemavu, ya kufundishia walimu na kusomea wanafunzi jambo ambalo limekuja
kuondoa tofauti ya Shule za binafsi na hizi za Serikali kwani kwa sasa shule
zinavutia zaidi kuliko za binafsi.
Ujenzi wa
Shule ya Sekondari Ntobo ulianza rasmi mwaka 2006, ni shule ya kutwa ambayo ni
mchanganyiko ambayo kwa sasa ina Kidato cha kwanza hadi cha nne na jumla ya
wanafunzi 577 sanjari na bweni la watoto wa kike lenye uwezo wa kuchukua wanafunzi
48.
Katika ziara
hiyo, Mhe Dejembi ameongozana na mwenyeji wake Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe.
Anamringi Macha, Mkuu wa Wilaya ya Kahama Mhe. Mboni Mhita, Mbunge wa Jimbo la
Msalala Mhe. Iddy Kassim Iddy.
Posted by MROKI
On Monday, October 07, 2024
No comments
0 comments:
Post a Comment