Nafasi Ya Matangazo

October 07, 2024

Ninawashukuru sana wadau wa Madini, Wachimbaji wakubwa, kati, wadogo na Wafanyabiashara ya Madini ambao kupitikia kikao cha pamoja katia yao na Benki kuu ya Tanzania (BOT) na Wizara ya Madini tumefikia muafaka katika maeneo meni na hivyo kuwezesha utekelezaji wa kifungu cha 59 cha Sheria ya Madini juu ya kutenga 20% ya uzalishaji wa dhahabu kwa ajili ya akiba ya nchi kupitia BOT.

MAMBO MUHIMU
i. Bei: Bei itakayotumika ni bei ya dhahabu duniani kama inavyotolewa na Tume ya Madini, hivyo bei hubadilika kila siku;

ii.Malipo: Asilimia 100 ya malipo baada ya kupokea ripoti ya uchenjuaji wa dhahabu; 

iii. Muda wa malipo: Ndani ya masaa 24 baada ya kupata ripoti ya uchenjuaji. Kwa miamala ya tarehe 02 Oktoba 2024, malipo yalifanyika ndani ya masaa sita;

iv. Gharama za kuchenjua: Benki Kuu italipia asilimia 100 ya gharama za kuchenjua dhahabu;

v. Asilimia 20 ya dhahabu: Hii inahusu mmiliki wa leseni ya chimbaji wa madini na mfanyabiashara mkubwa wa madini;

vi. Motisha: Mrabaha asilimia 4 badala ya asilimia 6; Ada ya ukaguzi ni asilimia 0 badala ya asilimia 1; na Kodi ya Ongezeko la Thamani asilimia 0, hivyo muuzaji wa dhahabu anaweza kudai "input tax”

vii. Chini ya mpango huu, wamiliki wa leseni ya uchimbaji wa madini, wafanyabiashara wakubwa wa madini na viwanda vya kuchenjulia dhahabu wanaweza kuluzia Benki Kuu kiasi chochote cha dhahabu.

Anthony Peter Mavunde
Waziri wa Madini
Posted by MROKI On Monday, October 07, 2024 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo