Nafasi Ya Matangazo

September 21, 2024

Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Dkt. Selemani Jafo,akikagua Mradi wa Usambazaji Maji vijiji 34 wilaya ya Ruangwa, vijiji 21 wilaya ya Nachingwea na kijiji 1 wilaya ya Lindi kwa kutumia chanzo cha maji cha mto Nyangao ikiwa ni mwendelezo wa ziara maalum wilaya ya Ruangwa Mkoani Lindi inayolenga kukagua utekekelezaji wa Miradi ya maendeleo katika Awamu ya Sita chini ya kauli mbiu isemayo "Rais Samia na Maendeleo Wasikie na Waone".
*******"" "
Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Dkt. Selemani Jafo, ametoa rai kwa wasimamizi wa maghala kupitia Mfumo wa Stakabadhi za Ghala kutoa huduma kwa uadilifu na uaminifu ili kuhakikisha mazao ya wakulima yanayohifadhiwa katika maghala hayo yanaingia na kutoka yakiwa na ujazo unaolingana ili kuvutia wafanyabiaashara wa ndani na nje kutumia Mfumo huo.

Vilevile Waziri Jafo ameendelea kuwasisitiza Wakulima kuhifadhi mazao yao katika mfumo wa stakabadhi za ghala yakiwa na ubora na kuacha tabia ya kuchanganya mqzao hayo na mazao mengine au mchanga hali inayosababisha mazao hayo kushindwa kuuzika katika soko la kimataifa na kuchafua taswira ya nchi ya Tanzania ambayo imeingia mikataba ya biashara baina ya nchi Jumuiya za Kikanda na Kimataifa.

Waziri Jafo, ameyasema hayo alipokagua, kuweka Jiwe la Msingi katika miradi mbalimbali ya maendeleo pamoja na kuongea na Wananchi wakati wa Ziara Maalum katika Wilaya ya Ruangwa Mkoa wa Lindi yenye lengo la kukagua utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo ikiongozwa na Kauli Mbiu isemayo "Rais Samia na Maendeleo Wasikie na Waone" iliyoanza tarehe 17 - 21/09/2024 Mkoani humo.

Aidha, akiwa ameridhishwa na utekelezaji wa miradi ya maendeleo wilayani humo, Waziri Jafo, alikagua ujenzi wa Mradi wa Usambazaji Maji unaujumisha Vijiji 56 vya Wilaya ya Ruangwa, Lindi na Nachingwe kutoka chanzo cha mto Nyangao (wilaya ya Lindi) na Ujenzi wa Barabara ya Mipingo yenye urefu wa Km. 0.78 pamoja na Chuo cha Ufundi Stadi VETA, na Kuzindua Mradi wa Jengo la ghorofa lenye madarasa 8, ofisi 4 na matundu 24 ya vyoo katika Shule ya Msingi Likangara.

Katika hatua nyinhine wakati akiongea na Wananchi wa Naipanga pamoja na Wafanyabiashara wa Soko la Matunda Wilayani humo, Waziri Jafo aliwahakikishia kuwa Serikali ya Awamu ya Sita itaendele kutatua changamoto mbalimbali walizonazo ili kuhakikisha kuwa huduma muhimu zinaendelea kutolewa kwa umma.

Aidha, amewashauri Wananchi wa Wilaya hiyo kulinda, kutunza na kutumia vyema majengo na vifaa mbalimbali vilivyoweka kupitia Miradi hiyo ya Maendeleo pamoja na kuongeza kasi ya kutafuta hati ya ardhi kwa baadhi ya miradi ili kuhakikisha wanaendelea kupata huduma bora za afya, elimu, maji na mingineyo.

Walinde miundombinu madarasa na wasichafue kuta.
Naye Mkuu wa Wilaya ya Ruangwa Mhe. Hassan ameishukuru Serikali ya Awamu ya Sita kwa kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo Wilayani humo na kuahidi kuwa Wilaya yake itasimamia itekelezaji wa maagizo yote yaliyotolewa ilinkuhakikisha Miradi yote ya Maendeleo Wilayani humo inakamilika kwa wakati na kuanza kitoa huduma kwa wananchi katika muda uliopangwa.

Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Dkt. Selemani Jafo,akizungumza na wananchi wa Nandagara waliompokea kwa shangwe wilaya ya Ruangwa wakati wa ziara Maalum wilayani humo inayolenga kukagua utekekelezaji wa Miradi ya Maendeleo katika Awamu ya Sita chini ya kauli mbiu isemayo "Rais Samia na Maendeleo Wasikie na Waone".

Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Dkt. Selemani Jafo,akizungumza na wananchi wa Nandagara waliompokea kwa shangwe wilaya ya Ruangwa wakati wa ziara Maalum wilayani humo inayolenga kukagua utekekelezaji wa Miradi ya Maendeleo katika Awamu ya Sita chini ya kauli mbiu isemayo "Rais Samia na Maendeleo Wasikie na Waone".
Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Dkt. Selemani Jafo,akizungumza na wananchi wa Nandagara waliompokea kwa shangwe wilaya ya Ruangwa wakati wa ziara Maalum wilayani humo inayolenga kukagua utekekelezaji wa Miradi ya Maendeleo katika Awamu ya Sita chini ya kauli mbiu isemayo "Rais Samia na Maendeleo Wasikie na Waone".
Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Dkt. Selemani Jafo,akikagua Mradi wa Usambazaji Maji vijiji 34 wilaya ya Ruangwa, vijiji 21 wilaya ya Nachingwea na kijiji 1 wilaya ya Lindi kwa kutumia chanzo cha maji cha mto Nyangao ikiwa ni mwendelezo wa ziara maalum wilaya ya Ruangwa Mkoani Lindi inayolenga kukagua utekekelezaji wa Miradi ya maendeleo katika Awamu ya Sita chini ya kauli mbiu isemayo "Rais Samia na Maendeleo Wasikie na Waone".
Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Dkt. Selemani Jafo,akikagua Mradi wa Usambazaji Maji vijiji 34 wilaya ya Ruangwa, vijiji 21 wilaya ya Nachingwea na kijiji 1 wilaya ya Lindi kwa kutumia chanzo cha maji cha mto Nyangao ikiwa ni mwendelezo wa ziara maalum wilaya ya Ruangwa Mkoani Lindi inayolenga kukagua utekekelezaji wa Miradi ya maendeleo katika Awamu ya Sita chini ya kauli mbiu isemayo "Rais Samia na Maendeleo Wasikie na Waone".
Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Dkt. Selemani Jafo,akikagua miundombinu ya Chuo cha Ufundi Stadi (VETA) ikiwa ni mwendelezo wa ziara maalum Mkoani Lindi inayolenga kukagua utekekelezaji wa Miradi ya maendeleo katika Awamu ya Sita chini ya kauli mbiu isemayo "Rais Samia na Maendeleo Wasikie na Waone".
Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Dkt. Selemani Jafo,akizungumza mara baada ya kukagua miundombinu ya Chuo cha Ufundi Stadi (VETA) ikiwa ni mwendelezo wa ziara maalum Mkoani Lindi inayolenga kukagua utekekelezaji wa Miradi ya maendeleo katika Awamu ya Sita chini ya kauli mbiu isemayo "Rais Samia na Maendeleo Wasikie na Waone".

Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Dkt. Selemani Jafo,akikagua miundombinu ya Chuo cha Ufundi Stadi (VETA) ikiwa ni mwendelezo wa ziara maalum Mkoani Lindi inayolenga kukagua utekekelezaji wa Miradi ya maendeleo katika Awamu ya Sita chini ya kauli mbiu isemayo "Rais Samia na Maendeleo Wasikie na Waone".

Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Dkt. Selemani Jafo,akiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi wa Veta ya Ruangwa mara baada ya kukagua miundombinu ya Chuo cha Ufundi Stadi (VETA) ikiwa ni mwendelezo wa ziara maalum Mkoani Lindi inayolenga kukagua utekekelezaji wa Miradi ya maendeleo katika Awamu ya Sita chini ya kauli mbiu isemayo "Rais Samia na Maendeleo Wasikie na Waone".
Posted by MROKI On Saturday, September 21, 2024 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo