Nafasi Ya Matangazo

September 07, 2024

Na Ofisi ya Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Mhe. Dkt. Doto Biteko Septemba 6, 2024 jijini Dodoma amekutana na kufanya mazungumzo na balozi mpya wa Uingereza nchini. Mhe. Marianne Young.

Lengo la mazungumzo hayo likiwa ni kujitambulisha kwa balozi huyo pamoja na kujadili masuala ya kipaumbele ya ushirikiano baina ya Tanzania na Uingereza katika sekta ya nishati.

Aidha katika mazungumzo hayo, Dkt.Biteko amepongeza ushirikiano mzuri uliopo baina ya Tanzania na Uingereza katika sekta mbalimbali hususan sekta ya nishati  kupitia ufadhili wa fedha kiasi cha shilingi bilioni 11.16 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ikiwemo Songas kupitia taasisi zake za mitaji za Shirika la UK Export Finance (UKEF) na Shirika la Uwekezaji la Uingereza (BII).

‘‘Serikali  itaendelea kushirikiana nanyi katika sekta ya nishati  sambamba na  kuikaribisha  sekta binafsi kutoka nchini Uingereza  kuja kuwekeza Tanzania  katika uzalishaji, uhifadhi na usambazaji wa nishati hususan nishati safi ya kupikia na nishati mbadala, ’’ amesema Dkt. Biteko.

Kwa upande wake, Balozi Young, ameipongeza Tanzania kwa uongozi wake katika kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia barani Afrika na kusema kuwa nchi yake itaendelea kuunga mkono sekta ya nishati nchini.

Mazungumzo hayo yamehudhuriwa pia na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki anayeshughulikia masuala ya Afrika Mashariki Mhe. Denis Londo.
Posted by MROKI On Saturday, September 07, 2024 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo