Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Mahmoud Thatib Kombo (Mb.) amepokea Nakala za Hati za Utambulisho kutoka kwa Balozi Mteule wa Rwanda nchini, Mhe. Jenerali Patrick Nyamvumba (kushoto). Mapokezi hayo yamefanyka katika Ofisi Ndogo za Wizara jijini Dar es Salaaam tarehe 5 Agosti, 2024.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Mahmoud Thatib Kombo (Mb.) akipokea Nakala za Hati za Utambulisho kutoka kwa Balozi Mteule wa Italia nchini, Mhe. Giuseppe Sean Coppola (Kushoto). Mapokezi hayo yamefanyika katika Ofisi Ndogo za Wizara jijini Dar es Salaaam tarehe 6 Agosti, 2024.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Mahmoud Thatib Kombo (Mb.) akipokea Nakala za Hati za Utambulisho kutoka kwa Balozi Mteule wa Zimbabwe nchini, Mhe. Helen Bawange Ndingani (Kushoto). Mapokezi hayo yamefanyika katika Ofisi Ndogo za Wizara jijini Dar es Salaaam tarehe 6 Agosti, 2024. ******************
Waziri wa Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Mahmoud Thatib Kombo (Mb.)
amepokea Nakala za Hati za Utambulisho kutoka kwa Balozi Mteule wa Zimbabwe
nchini, Mhe. Helen Bawange Ndingani, Balozi Mteule wa Italia nchini, Mhe.
Giuseppe Sean Coppola na Balozi Mteule wa Rwanda nchini, Mhe. Jenerali Patrick
Nyamvumba katika Ofisi Ndogo za Wizara jijini Dar es Salaaam tarehe 6 Agosti,
2024.
Akipokea nakala hizo Waziri
Kombo amewapongeza mabalozi hao kwa uteuzi waliuopata na pia amewaahidi
ushirikiano katika utekelezaji wa majukumu yao kwa kipindi watakachokuwa nchini
kuziwakilisha nchi zao.
Aidha, ameeleza Mabalozi hao
Wateule wanatarajiwa kuwasilisha Hati za Utambulisho kwa Mhe. Dkt. Samia Suluhu
Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tarehe 12 na 13 Agosti, 2024.
Akiongea na Balozi Mteule wa
Zimbambwe nchini, Mhe. Ndingani, Waziri Kombo ameeleza kuwa Tanzania na
Zimbabwe zimekuwa na ushirikiano wa kihistoria na kindugu ulioasisiwa na
waasisi wa mataifa hayo mawili Hayati, Mwl. Julius Kambarage Nyerere wa
Tanzania na Hayati, Robert Mugabe wa Zimbabwe.
Vilevile, akamkaribisha Mhe.
Ndingani kutembelea Maktaba ya Hayati Mwl. Nyerere iliyopo Butiama, mkoani Mara
ambayo imesheheni historia yake.
Balozi Kombo pia, akaeleza
umuhimu wa kuwekeza na kurithisha historia ya ukombozi kwa vijana ili waweze
kufahamu kwa kina namna waasisi hao walivyojitoa kupigania uhuru wa Bara la Afrika
hususan harakati za ukombozi wa nchi za Kusini mwa Afrika.
Viongozi hao pia jadili juu ya
umuhimu wa kufanyika kwa Mkutano wa Tume ya Pamoja ya Ushirikiano (JPC) kati ya
Tanzania na Zimbabwe ambapo ameeleza kuwa Tanzania inatarajia kuwa mwenyeji wa
mkutano huo. Tanzania na Zimbabwe zinashirikiana katika masuala ya biashara,
uwekezaji, usafirishaji, usalama wa chakula, mabadiliko ya tabia nchi, elimu,
Sanaa na utamaduni, na sekta nyingine za kisiasa.
Akizungumza na Balozi Mteule
wa Italia nchini, Mhe. Coppola, Mhe. Waziri Kombo amesisitiza kuwa Tanzania ina
nia ya dhati ya kuendeleza ushirikiano na nchi hiyo ili kuwezesha utekelezaji
wa miradi ya kimkakati kupitia mpango wa ushirikiano wa Italia na Afrika
unaofahamika kama “Mattei Plan”. Tanzania na Italia zinashirikiana katika sekta
za utalii, elimu, Maji, biashara na uwekezaji, kilimo, mifugo na uvuvi, na
kuongeza thamani ya mazao yatokanayo na ngozi ili kukuza biashara yake
kimataifa.
Tanzania na Italia zinatarajia
kuwa na Kongamano la biashara litakalofanyika jijini Dar es Salaam mwezi
Desemba, 2024 kwa lengo la kukuza sekta ya biashara na za kiuchumi kwa maslahi
mapana ya pande zote mbili amabapo, pembezoni mwa kongamano hilo kutafanyika
mashauriano ya kisiasa.
Vilevile, katika mazungumzo
yake na Balozi wa Rwanda, Mhe. Jenerali, Patrick Nyamvumba, Mhe. Waziri Kombo
ameeleza kuwa Tanzania itaendelea kushirikiana na Rwanda kupitia ujirani wa
nchi hizo mbili sambamba na kusimamia makubaliano mbalimbali yaliyokubaliwa
katika nyakati tofauti na majukwaa mbalimbali ambayo nchi hizo mbili
zimekubaliana kuyatekeleza.
Tanzania na Rwanda
zinashirikiana katika sekta za mawasiliano, biashara na uwekezaji,
usafirishaji, elimu, utamaduni na michezo, miundombinu, kilimo na mifugo.
Jukumu hili la kupokea Nakala
za Hati za Utambulisho limefanywa na Mhe. Waziri Kombo kwa mara ya kwanza tangu
aapishwe na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu
Hassan kushika nafasi ya Waziri wa Mambo ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa
Afrika Mashariki.
0 comments:
Post a Comment