Wakati zoezi la uhakiki, usasishaji na usajili wa Anwani za Makazi likiendelea katika Halmashauri sita za Mkoa wa Arusha, Halmashauri ya Monduli imefanikiwa kufikia asilimia 22.77 ya usasishaji anwani za makazi ndani ya siku 5 kutoka Agosti 17 hadi 21 mwaka huu 2024.
Akizungumzia maendeleo ya zoezi hilo ofisini kwake tarehe 21 Agosti, 2024, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Monduli, Bi Happiness Laizer, amesema Anwani zilizosasishwa hadi leo mchana ni 6621 kati ya 29,082 zilizosajiliwa mwaka 2022.
Bi. Laizer amesema anwani mpya zilizosajiliwa ni 1,358 sawa na ongezeko la asilimia 4.67 yakiwa ni mafanikio makubwa kwa eneo hilo linalokaliwa na jamii ya Kimasai.
Waratibu wa Anwani za Makazi Taifa walipotembelea Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Monduli Bi. Happiness Laizer, tarehe 21 Agosti, 2024.
Pamoja na mambo mengine wamezungumzia zoezi la Uhakiki, Usasishaji wa Anwani za Makazi na Usajili wa Anwani mpya linaloendelea pamoja na matumizi ya Mfumo wa programu Tumizi ya NaPA na huduma ya Barua ya Utambulisho Kidigitali.
Waratibu wa Anwani za Makazi Taifa walipotembelea Kaburi la Hayati Edward Lowassa aliyekuwa Waziri Mkuu Mstaafu katika Serikali ya Awamu ya Nne lililopo nyumbani kwake Kijiji cha Ngarashi, Halmashauri ya Wilaya ya Monduli.
Timu hiyo ya wataalamu ikifika katika makazi ya kiongozi huyo wakati wa zoezi la Uhakiki wa Anwani za Makazi linaloendelea katika kijiji hicho tarehe 21 Agosti, 2024.
Waratibu wa Anwani za Makazi Taifa walipotembelea makazi ya Waziri Mkuu Mstaafu Hayati Edward Moringe Sokoine yaliyopo katika Kata ya Monduli Juu, Halmashauri ya Wilaya ya Monduli.
Wataalam hao walipata nafasi hiyo wakati wakikagua maendeleo ya zoezi la Uhakiki wa Anwani za Makazi ambapo walipata nafasi ya kutembelea Kaburi la Kiongozi huyo lililopo nyumbani kwake tarehe 21 Agosti, 2024.
0 comments:
Post a Comment