Nafasi Ya Matangazo

July 22, 2024

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akiangalia moja ya mashati yaliyoshonwa na Kikundi cha Wazazi cha  Wajasiriamali baada ya kuzindua kikundi hicho  kilichopo eneo la Kilimani ambapo kikundi hicho kinajishughulisha na shughuli za ushonaji, utengenezaji sabuni na biashara mbalimbali.Tukio hilo la ufunguzi limefanyika leo Visiwani Zanzibar.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
Katibu wa  Kikundi cha Wazazi cha  Wajasiriamali,Hawa Said akionyesha kiasi cha Shilingi Milioni Moja walizopewa na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,Mhandisi Hamad Masauni(kushoto) kwa ajili ya mchango baada ya Waziri kuzindua kikundi hicho kinachojishughulisha na shughuli za ushonaji, utengenezaji sabuni na biashara mbalimbali.Tukio hilo la ufunguzi limefanyika leo Visiwani Zanzibar.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akiangalia moja ya kikapu kilichotengenezwa na Kikundi cha Wazazi cha  Wajasiriamali baada ya kuzindua kikundi hicho  kilichopo eneo la Kilimani ambapo kikundi hicho kinajishughulisha na shughuli za ushonaji, utengenezaji sabuni na biashara mbalimbali.Tukio hilo la ufunguzi limefanyika leo Visiwani Zanzibar.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (aliyeshika mkasi), akikata utepe kuzinduzi Kikundi cha Wazazi Wajasiriamali kilichopo eneo la Kilimani ambapo kikundi hicho kinajishughulisha na shughuli za ushonaji, utengenezaji sabuni na biashara mbalimbali.Tukio hilo la ufunguzi limefanyika leo Visiwani Zanzibar.Wengine pichani ni viongozi mbalimbali wa Jimbo la Kikwajuni waliohudhuria hafla hiyo.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

Na Mwandishi Wetu,Zanzibar
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,Mhandisi Hamad Masauni amewaonya wanafunzi walioko mashuleni,vyuoni na taasisi nyingine za elimu kuacha na kutojihusisha na matumizi ya dawa za kulevya kwani kushiriki katika matumizi ya dawa hizo itapelekea nchi kupoteza nguvu kazi ambayo inategemewa katika kujenga taifa huku akiitaka jamii kushirikiana na serikali katika vita dhidi ya dawa za kulevya.
 
Ametoa kauli hiyo wakati akizungumza katika mkutano wa hadhara baada ya kufungua Kikundi cha Ujasiriamali kilichopo Visiwani Zanzibar ambacho kinajumuisha makundi mbalimbali ikiwemo kundi la vijana ambalo limekua likiathirika na matumizi ya dawa za kulevya ambapo wamekua wanatumia kwa njia ya kuvuta puani,kuvuta mdomoni na kujidunga sindano.
 
‘Ni muhimu kwa jamii nzima kushikamana ili kuweza kupambana na matumizi ya dawa za kulevya,tafiti zinaonyesha sasa janga la matumizi ya dawa za kulevya limehamia kwa wanafunzi ambao wengine wana digrii zao lakini wamejiingiza katika uraibu wa dawa za kulevya,jambo hili linahatarisha uhai wa taifa kwani vijana ni nguvu kazi ya taifa lolote lile duniani,sisi kwa upande wa serikali tumeunganisha nguvu ya pamoja katika kudhibiti uingiaji wa dawa za kulevya na wito wangu kwa wazazi na wanajamii kuhakikisha wanashirikiana na serikali katika kudhibiti janga hilo’ amesema Waziri Masauni
 
Waziri Masauni pia amezungumzia matendo ya udhalilishaji ikiwemo ulawiti,ubakaji,ushoga ambayo yanaendelea kukithiri huku jamii pamoja na familia wakiendelea kuwaficha watu wenye kujihusisha na matendo hayo ambapo ameiasa jamii kutoa taarifa kwa Jeshi la Polisi waonapo dalili za udhalilishaji wa kijinsia kwa watoto na makundi mbalimbali.
 
‘Kuna mmomonyoko wa maadili unaopelekea matukio ya ukiukwaji wa maadili hayo ikiwemo unyanyasaji wa kijinsia,ubakaji,ulawiti na ushoga;mambo hayo hayajaisha katika jamii yetu na ni muhimu kwa jamii nzima kushikamana ili kupambana na majanga haya,na kumekua na desturi kwa baadhi ya watu wanaofanya matendo ya ubakaji na ulawiti hususani ya watoto tunawakumbatia na kuwaficha,imefikia hatua mtu amethibitika kufanya ulawiti lakini wanamficha katika kuhakikisha yule mtuhumiwa aendi kwenye mikono ya sheria hiyo sio sawa.’ Aliongeza Waziri Masauni
 
Taarifa  zinabainisha walevi wa uraibu wa dawa za kulevya wamekuja na mtindo wa kutumia dawa za kutibu binadamu kama mbadala wa dawa za kulevya huku wakichukua dawa aina ya methamphetamine ambayo waraibu uchukua dawa hiyo kuisaga na kuiweka kwenye kijiko huku mshumaa ukitumika kuipasha na mwisho mraibu huvuta moshi unaotokana na uunguaji wa dawa hiyo.
Posted by MROKI On Monday, July 22, 2024 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo