Mbunge wa Jimbo la Solwa, Halmashauri ya Shinyanga, wilayani Shinyanga, Mhe. Ahmed Salim, amempongeza Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga, Wakili @julius_mtatiro kwa kumwita "DC wa kipekee ambaye hajawahi kutokea katika wilaya hiyo..."
Mbunge Ahmed amekiri hayo wakati akitoa salamu zake katika Kikao Maalum cha Halmashauri Kuu ya CCM wilaya ya Shinyanga Vijijini, ambapo pamoja na mambo mengine amekiri kuwa tangu Mtatiro ahamishiwe Shinyanga, akitokea Tunduru mkoani Ruvuma, amekuwa kiungo muhimu, chachu ya kuunganisha Ofisi za Wabunge na Serikali katika kuwahudumia wananchi; Kufanya mikutano mingi ya utatuzi wa kero za wananchi, na kuendesha kliniki nyingi za utatuzi wa migogoro iliyoshindikana kwa miaka mingi ndani ya wilaya.
Mbunge Ahmed ametolea mfano suala la bei kubwa za maji katika kata za Didia, Tinde na Iselamagazi ambapo kwa miaka mitatu mfululizo wananchi wa kata hizo walikuwa wananunua maji kwa shs 2,550 kwa uniti 1 huku wale wa Mjini na maeneo mengine wakinunua kwa shs 1,450 kwa uniti 1.
Mbunge Ahmed amesema, Mtatiro alipofika Shinyanga aliweka msimamo wa wazi kupinga suala hilo la kiuonevu na kwamba Mtatiro aliunganisha nguvu za wabunge na akalisimamia kisheria na Waziri wa Maji Jumaa Awesso akasaidia kulitatua kwa wakati.
Mbunge Ahmed amesisitiza, kama asingalikuwa Mtatiro kuunganisha nguvu za serikali na wawakilishi wa wananachi, jambo hilo lisingelifika mwisho.
Wajumbe katika kikao cha Halmashauri Kuu wakiwemo madiwani wa Shinyanga, wamempongeza Wakili Mtatiro kwa kasi yake ya utendaji, ufanyaji maamuzi, ufufuaji wa timu ya Stand United kimkoa, kauli njema na zenye utu kwa wananchi, na mapambano yake dhidi ya wakandarasi na watumishi wazembe na wasiotimiza wajibu huo.
Halmashauri Kuu ya CCM Wilaya ya Shinyanga Vijijini imesisitiza kuwa itamuunga mkono Mtatiro kwa hali na Mali.
Shinyanga.
0 comments:
Post a Comment