Nafasi Ya Matangazo

July 12, 2024







Uongozi wa Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ) ukiongozwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Benki hiyo, Josephat Meza na Afisa Mtendaji Mkuu Arafat Haji wako nchini Comoro ambapo wamefanya mazungumzo na Gavana wa Benki Kuu ya Comoro, Mhe. Dkt Younoussa Imani kwa maeneo mbalimbali ya ushirikiano.


Uongozi wa Benki hiyo wameambatana na Balozi wa Tanzania nchini Comoro, Saidi Yakubu na pande hizo mbili zimekubaliana maeneo mbali mbali ya ushirikiano.

Benki ya Watu wa Zanzibar ni miongoni mwa benki zinazotambuliwa na Benki Kuu ya Tanzania kama Benki Kubwa na ndiyo inayoongoza kwa operesheni za kibenki visiwani Zanzibar ikiwa imeanzishwa miaka 58 iliyopita na ina matawi 35 nchini kote Tanzania.
Posted by MROKI On Friday, July 12, 2024 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo