Nafasi Ya Matangazo

June 12, 2024
Mkuu wa Mkoa wa Singida Halima Dendego, amekataa kuzindua bweni la Wanafunzi wa kike katika shule ya Sekondari Mtekente iliyopo Wilayani Iramba baada ya kubaini kuwa ujenzi huwa wa bweni pamoja na jiko yaliyojengwa na Kampuni inayojishughulisha na ununuzi wa pamba Biosustain mkoani humo kwa zaidi ya shilingi milioni 180 yamejengwa chini ya Kiwango.

Kufutia hali hiyo, Mkuu huyo wa Mkoa wa Singida amemwagiza Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Iramba kushirikiana na Kampuni hiyo katika kurekebisha maeneo yote yenye kasoro ikiwemo sakafu ndipo ataenda kuzindua bweni hilo ambayo yatakuwa na uwezo wa kuchukua wanafunzi wa kike 80 kabla ya shule kufunguliwa.

Amesema ujenzi huo wa bweni limejengwa vizuri lakini umaliziaji ndio mbovu katika maeneo mbalimbali ikiwemo kwenye kuta na vyoo hivyo kazi ya maboresho lazima ifanyike haraka kabla ya wanafunzi kurejea mashuleni.

Halima Dendego amewasisitiza Viongozi katika ngazi zote kuhakikisha wanashiriki kikamilifu katika usimamizi wa miradi kama hiyo hata kama ni ya wafadhili ili kazi iweze kufanyika kwa viwango vinavyotakiwa kulingana na thamani ya fedha.

Kuhusu tatizo la Walimu wa shule ya Sekodari Mtekente kutishiwa maisha ya baadhi ya wananchi wa kijiji hicho, Mkuu wa wa mkoa wa Singida Halima Dendego amemwagiza Mkuu wa Polisi wa Wilaya ya Iramba kuchukua hatua haraka za kuwakamata na kuwachukulia hatua wananchi wanaowatishia maisha walimu hao ili kukomesha vitendo hivyo.

Halima Dendego amesema kuwa anataka kuona Watumishi waliopo mkoani Singida wanafanya kazi kwa amani bila kusumbuliwa na mtu yeyote na atakayewasumbua basi lazima awajibishwe kwa kuchukuliwa hatua za kisheria.

“Nendeni Mkawaambie Vijana wetu huko mtaani nikiona tukio la namna hii linajitokeza tena nitajua la kufanya na msije mkanilaumu, Amesisitiza Halima Dendego.

Mkuu huyo wa mkoa pia amewataka Walimu waendelee kufanya kazi kwa bidii kwa sababu Serikali inajua changamoto wanazokumbana nazo ikiwemo madai yao na Serikali itaendelea kuzitatua changamoto hizo kwa muda muafaka.

Imetolewa na 
Kitengo cha Mawasiliano Ofisi ya 
Mkuu wa mkoa wa Singida.
0755 516 591.
0712 762 097
PTC . 1. Mkuu wa mkoa wa Singida Halima Dendego akizungumza mara baada ya kukagua mradi wa ujenzi wa bweni la Wanafunzi wa Kike katika shule ya Sekondari Mtekente wilayani Iramba.

PTC. 2. Mkuu wa mkoa wa Singida Halima Dendego akizungumza na wanafunzi wa shule ya Sekondari ya Mtekente wilayani Iramba.

PTC 3. Jengo la bweni la Wanafunzi wa Kike katika shule ya Sekondari ya Mtekente ambalo Mkuu wa mkoa wa Singida Halima Dendego amekataa kulizindua mpaka lifanyiwe marekebisho.

PTC 4. Mkuu wa mkoa wa Singida Halima Dendego akiwa kwenye ukaguzi wa ndani ya bweni.

PTC 5. Mwonekano wa bweni la Wasichana kwa ndani katika shule ya Sekondari Mtekente wilayani Iramba.
PTC 6. Vitanda vilivyopo katika bweni la Wasichana shule ya Sekondari ya Mtekente wilayani Iramba.

PTC. 7Mkuu wa mkoa wa Singida Halima Dendego akiwa kwenye ukaguzi wa bweni la Wasichana Mtekente wilayani Iramba.
Posted by MROKI On Wednesday, June 12, 2024 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo