Nafasi Ya Matangazo

June 22, 2024

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye mazungumzo na Mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Guinea-Bissau Mhe. Umaro Sissoco Embaló, Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 22 Juni, 2024.
Rais wa Jamhuri ya Guinea-Bissau Mhe. Umaro Sissoco Embaló akisaini Kitabu cha Wageni mara baada ya kuwasili Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 22 Juni, 2024.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa Mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Guinea-Bissau Mhe. Umaro Sissoco Embaló mara baada ya kuwasili Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 22 Juni, 2024.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Rais wa Jamhuri ya Guinea-Bissau Mhe. Umaro Sissoco Embaló, Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 22 Juni, 2024.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimkabidhi mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Guinea-Bissau Mhe. Umaro Sissoco Embaló zawadi ya vitabu vya Lugha ya Kiswahili mara baada ya kuwasili Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 22 Juni, 2024.
****************
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan anatarajia kumpokea Rais wa Jamhuri ya Guinea-Bissau, Mhe.  Umaro Sissoco Embaló tarehe 22 Juni, 2024 Ikulu jijini Dar es Salaam ambae atakuwa nchini kwa ziara ya kikazi.

 
Hii ni mara ya kwanza kwa Rais wa Guinea-Bissau kufanya ziara nchini Tanzania tangu nchi hiyo ipate uhuru.

Ziara hiyo itatoa fursa kwa nchi zote mbili kuimarisha ushirikiano na uhusiano ambao umedumu kwa muda mrefu ulioasisiwa na Hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na Hayati Amilcar Cabral wa Guinea-Bissau wakati wa kupigania uhuru.

 
Wakati wa ziara hiyo, Marais hao wawili wanatarajia kuongoza mazungumzo rasmi ya kiserikali kati ya Tanzania na Guinea-Bissau na kushuhudia utiaji saini wa Mkataba wa Ushirikiano (General Framework Agreement) ambao utaongeza mahusiano kati ya nchi hizi mbili.
 
Mbali ya mazungumzo na Rais Samia, Rais Embaló atatembelea Mradi wa Reli ya Kisasa (SGR), Eneo Huru la Uwekezaji kwa Mauzo ya Nje (EPZA) na Makao Makuu ya Sekretarieti ya Taasisi ya Viongozi wa Afrika ya Kukabiliana na Ugonjwa wa Malaria (ALMA) yaliyopo hapa nchini, ambapo yeye ni Mwenyekiti wa ALMA.  

Posted by MROKI On Saturday, June 22, 2024 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo