Kamati ya maendeleo ya kata mjimwema (WDC) kiongozwa na Mwenyeki wake Mhe, Omary Ngurangwa pamoja na uongozi wa chama cha mapinduzi, na leo June,26,2024 wamefanya ziara ya kutembelea miradi mbalimbali ya maendeleo katika kata inayotekelezwa na fedha za mapato ya ndani ya Halmashauri na fedha kutoka serikali kuu.
Ziara iyo imetembelea na kukagua miradi ifuatayo: bweni shule ya Sekondari kidete,Vyumba vya madarasa viwili katika Shule za Msingi Mjimwema na Kibugumo
kukagua Ujenzi wa uzio na Nyumba ya mtumishi katika Zahanati ya Kibugumo, pia imetembelea Ujenzi , Ofisi ya serikali ya mtaa Ungindoni pamoja na Kituo cha Afya cha gorofa nne kinachojengwa katika eneo la kisota mtaa wa Mjimwema, Kituo hicho cha kimkakati na cha aina yake kinajengwa Kwa mapato ya fedha za ndani za halmashauri ya manispaa Kigamboni.
Mhe, Omary Ngurangwa ametoa shukrani zake za dhati kwa Mhe,Rais Dr. Samia Suluhu Hasaan Kwa kuendelea Kutoa fedha mbalimbali za miradi katika Kata ya Mjimwema na wilaya ya Kigamboni Kwa Jumla
"Lengo la Ziara hii kwanza kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo katika Kata yetu tunamshukuru na tunatambua Mhe,Rais Dkt Samia Suluhu Hasaan amekuwa akitoa fedha nyingi za miradi ya maendeleo na Ofisi ya mkurugenzi halmashauri ya manispaa ya kigamboni imekuwa ikitoa fedha Kwajili ya miradi pia.
Aidha kipekee naomba nitoe shukrani zangu Mbunge wa kigamboni Mhe. Dr. Ndugulile, Baraza la madiwani la manispaa ya kigamboni na Ofisi ya mkurugenzi Kwa kuridhia na kupitisha bajeti ya Ujenzi wa kituo cha afya katika kata ya Mjimwema kiukweli wakina mama walikuwa wanaenda kujifungulia katika kata za vijibweni au kigamboni ila kwa sasa hili tatizo litakwisha Ujenzi utakapokamilika,, Alisema Diwani wa Mjimwema Mhe,Omari Ngurangwa.
"Mimi Siyo Mjumbe wa kamati ya maendeleo ya Kata ila nampongeza mwenyekiti wa kamati hii Kwa kunipa mualiko wa kujumuika pamoja na kufanya Ziara ya ukaguzi wa miradi mbalimbali ya maendeleo Rais wetu amekuwa akitoa fedha nyingi za kutekeleza miradi pia niwaombe watumishi wa serikali kushirikiana na wananchi mara baada serikali inapoleta fedha za miradi,, Alisema ndugu Kassim Issa Abdallah mwenyekiti wa chama cha mapinduzi Kata ya Mjimwema.
0 comments:
Post a Comment