Nafasi Ya Matangazo

June 08, 2024

Mbunge mteule wa Jimbo la Kwahani Wilaya ya Mjini, Mkoa wa Mjini Magharib, Zanzibar, Bw.Khamis Yussuf Mussa akinyanyua juu hati yake ya ushindi baada ya kukabidhiwa na Msimamizi wa Uchaguzi. 
Mbunge mteule wa Jimbo la Kwahani Wilaya ya Mjini, Mkoa wa Mjini Magharib, Zanzibar, Bw.Khamis Yussuf Mussa akionesha hati yake ya ushindi baada ya kukabidhiwa na Msimamizi wa Uchaguzi.
Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Kwahani, Zanzibar Bi.Safia Iddi Muhammad akimkabidhi hati ya ushindi Bw.Khamis Yussuf Mussa kutoka Chama Cha Mapinduzi (CCM) baada ya kumtangaza kuwa ndiye mshindi wa Kiti cha Ubunge katika Jimbo la Kwahani.
Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Kwahani, Zanzibar Bi.Safia Iddi Muhammad akisoma matokeo ya Jimbo la Kwahani. 
Wagombea na mawakala wao wakifuatilia matokeo hayo.
Aliyekuwa Mgombea wa CCM, 
Bw.Khamis Yussuf Mussa 'Pele' akifuatilia kwa makini utangazaji wa matokeo. 
Wagombea na mawakala wao wakifuatilia matokeo hayo.

Wananchi wakisubiri matokeo.
Waangalizi wa Uchaguzi wa Kwahani wakisikiliza matokeo.
*************
Na Mwandishi wetu, Zanzibar
Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) kupitia Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Kwahani-Zanzibar Bi.Safia Iddi Muhammad imemtangaza Bw.Khamis Yussuf Mussa kutoka Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuwa mshindi wa Kiti cha Ubunge katika Jimbo la Kwahani.
 
Mussa almaarufu Pele ameibuka mshindi wa kiti hicho baada ya kupata Kura 7,092 Kati ya Kura halali 7,383 zilizopigwa na kuwabwaga wagombea wenzake 13 waliokuwa wakichuana katika uchaguzi mdogo wa jimbo hilo uliofanyika leo tarehe 8 Juni, 2024.
 
Jimbo la Kwahani lilikuwa na wapiga kura 11,936 na waliojitokeza kupiga kura ni 7,522 ambapo kura 139 zilikataliwa hivyo kufanya kura halali zilizopigwa kuwa ni 7,383.
 
Vyama 14 vilisimamisha wagombea katika Uchaguzi huo mdogo wa kiti cha Ubunge jimbo la Kwahani lililopo Wilaya ya Mjini Mkoa wa Mjini Magharibi.
 
Wagombea wengine na kura walizopata katika mabano ni pamoja na Bi. Jarade Ased Khamis  wa AAFP (06), Bi. Madina Mwalim Hamad wa ADA TADEA (49), Bi. Shara Amran Khamis  wa ADC (83), Bi. Zainab Maulid Abdallah  wa CCK (21), Bw. Abdi Khamis Ramadhan wa CUF(79), Bw.  Bashir Yatabu Said  wa Demokrasia Makaini (14) 
na Bi. Nuru Abdulla Shamte  wa DP(07) .
 
Wengine ni 
Bw. Kombo Ali Juma  wa NRA (05), Bi. Mwanakombo Hamad Hassan  wa NLD (08),  Bw. Amour Haji Ali  wa SAU(07), Bi. Naima Salum Hamad  wa UDP(01), Bi. Mashavu Alawi Haji  wa UMD(05) na Bi. Tatu Omary Mungi  wa UPDP(06).
 
Uchaguzi katika Jimbo la Kwahani umefanyika kufuatia kifo cha aliyekuwa Mbunge wa Jimbo hilo kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), Ahmed Yahya Abdulwakil (65) kufariki dunia mwezi Aprili mwaka huu.
 
 
Posted by MROKI On Saturday, June 08, 2024 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo