Nafasi Ya Matangazo

May 12, 2024

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akitazama Kakao alipotembelea shamba la Mkulima zao hilo Clement Msalangi lililopo kijiji cha Mababu, Wilayani Kyela Mei 12, 2024.  Kulia kwake ni mkewe Mama Mary Majaliwa.  Mheshimiwa Waziri Mkuu yupo Mkoani Mbeya kwa ziara ya kikazi. 


Waziri Mkuu Kassim Majaliwa  akizungumza na Naibu Waziri wa Kilimo, David Silinde alipotembelea shamba la Mkulima wa  Kakao,  Clement Msalangi lililopo kijiji cha Mababu, Wilayani Kyela Mei 12, 2024. Kulia kwake ni Mkewe Mama Mary Majaliwa, na kilia ni Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Juma Homera. Mheshimiwa Waziri Mkuu yupo Mkoani Mbeya kwa ziara ya kikazi.
***********
Waziri Mkuu Kasssim Majaliwa leo Mei 12, 2024 ametembelea shamba la Mkulima zao la Kakao Clement Msalangi lililopo kijiji cha Mababu, Wilayani Kyela Mei 12, 

Akizungumza baada ya kulitembelea Mheshimiwa Majaliwa amewataka wakulima wa zao hilo wajisajili na watambue idadi ya miche waliyonayo na ukubwa wa mashamba yao ili wakati Serikali ikitoa ruzuku kila mkulima anufaike na kuiwezesha Serikali kujua ni tani kiasi gani itazalishwa.

Aidha, Waziri Mkuu amewataka wakulima na viongozi wa AMCOS wasimamie ubora zao la Kakao na kuzitumia fedha wanazopata baada ya mauzo kujiletea maendeleo katika maeneo yao.
Posted by MROKI On Sunday, May 12, 2024 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo