Mhashamu
Askofu Msaidizi wa Jimbo Kuu Katoliki Dodoma Wilbroad Kibozi akiwekwa Wakfu na
kukabidhiwa mavazi na fimbo ya kiaskofu katika sherehe iliyofanyika Kituo Cha
Hija Miyuji Mbwanga mkoani Dodoma tarehe 12 Mei 2024.
Makamu wa Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip
Mpango na Mwenza wake Mama Mbonimpaye Mpango wakiwa
wameungana na waumini pamoja na viongozi mbalimbali kushiriki adhimisho la Misa
Takatifu wakati wa Sherehe ya Kuwekwa Wakfu Mhashamu Askofu Msaidizi wa Jimbo
Kuu Katoliki Dodoma Wilbroad Kibozi iliyofanyika Kituo Cha Hija Miyuji Mbwanga
mkoani Dodoma tarehe 12 Mei 2024.
Mhashamu Askofu Msaidizi wa Jimbo Kuu Katoliki Dodoma Wilbroad Kibozi
akiwekwa Wakfu na kukabidhiwa mavazi na fimbo ya kiaskofu katika sherehe
iliyofanyika Kituo Cha Hija Miyuji Mbwanga mkoani Dodoma tarehe 12 Mei 2024.Mhashamu Askofu Msaidizi wa Jimbo Kuu Katoliki Dodoma Wilbroad Kibozi akiwekwa Wakfu na kukabidhiwa mavazi na fimbo ya kiaskofu katika sherehe iliyofanyika Kituo Cha Hija Miyuji Mbwanga mkoani Dodoma tarehe 12 Mei 2024.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akizungumza na Maaskofu, Mapadre, Watawa, Viongozi wa Serikali pamoja na Waumini mbalimbali mara baada ya kumalizika kwa Ibada ya kuwekwa Wakfu Mhashamu Askofu Msaidizi Wilbroad Kibozi iliyofanyika Kituo Cha Hija Miyuji Mbwanga mkoani Dodoma tarehe 12 Mei 2024.
***************
Makamu wa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango ametoa wito kwa
Wazazi na Walezi nchini kuongeza jitihada katika malezi na makuzi bora ya
watoto ili kukabiliana na changamoto ya ukatili unaowezeshwa na mitandao unaotishia usalama wa watoto ambapo
watoto wanarubuniwa ili kujihusisha na vitendo viovu.
Makamu wa
Rais ametoa wito huo wakati alipomwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania katika Ibada ya kuwekwa Wakfu Askofu Msaidizi wa Jimbo Kuu Katoliki Mhashamu
Askofu Wilbroad Kibozi iliyofanyika Kituo Cha Hija Miyuji Mbwanga mkoani
Dodoma. Amewasihi wazazi na walezi kutenga muda kujenga urafiki na watoto, ili
kufahamu maendeleo yao, marafiki zao, na kuwawezesha kuwa huru kueleza
changamoto zozote wanazopitia na hivyo kuweza kuwasaidia mapema.
Amesema
matumizi mabaya ya maendeleo ya teknolojia ya habari na mawasiliano, na mwingiliano holela wa mila na desturi za
mataifa mbalimbali zimeendelea kuathiri malezi na makuzi ya watoto pamoja na
kudhoofika muunganiko wa kindugu au kirafiki kati ya wazazi na watoto wao ambao
umepelekea watoto kukosa upendo na ulinzi wa wazazi au walezi.
Aidha Makamu
wa Rais amehimiza vijana kufanya kazi kwa bidii ili kujipatia kipato halali
kitakacho wawezesha kujikimu kimaisha. Amesema ni vema vijana wakajikita katika
kazi za staha bila kuchagua zikiwemo za kilimo cha mbogamboga na matunda, na
ufugaji wa wanyama aina mbalimbali za ndege na viumbe maji. Pia ametoa rai kwa
watanzania kuzingatia muda wakati wa kuzalisha mali na utoaji huduma ili
kuongeza kasi ya ukuaji wa Pato la Taifa na la mtu mmoja mmoja.
Halikadhalika
Makamu wa Rais amewasihi viongozi wa Dini kuendelea kuhamasisha usafi, upandaji
miti na utunzaji wa mazingira bila kuchoka na kuwaomba kukemea utupaji hovyo wa
taka, uchomaji wa misitu na ukataji hovyo wa miti hususan kwa kutumi misumeno
ya mnyororo ambayo imegeuka kuwa silaha mbaya ya kuangamiza misitu.
Aidha
amesisitiza suala la Taasisi zote za umma na za kidini (zikiwemo nyumba za
Watawa, Seminari, Shule na Vyuo) ambazo zinalisha zaidi ya watu 100 kwa siku,
kuhama kutoka matumizi ya nishati chafu, yaani mkaa na kuni, kwa ajili ya
kupikia na kuanza kutumia nishati safi, yaani gesi asili, bio gas na umeme ili
kufikia lengo la Taifa la 80% ya
Watanzania wawe wanatumia nishati safi ya kupikia ifikapo 2034.
Makamu wa
Rais amesema Serikali inathamini mchango mkubwa wa Kanisa Katoliki, na
madhehebu mengine ya Dini, katika utoaji wa huduma za kijamii na malezi bora.
amesema Serikali itaendelea kusimamia na kulinda haki ya kuabudu kwa wananchi
wote kwa mujibu wa Katiba na kuhakikisha wananchi wanaendelea kuishi katika
mazingira ya haki na amani.
Makamu wa Rais ameongeza kwamba Kanisa na
madhehebu mengine ya Dini ndiyo dhamiri ya jamii hivyo ni vyema Viongozi wa
Dini kuishi wito wa kinabii kwa kusema na kuutetea ukweli kwa ajili ya maslahi
ya wananchi hasa wanyonge.
Aidha
amewasihi kuendelea kuwakumbusha waamini na Watanzania kwa ujumla kwamba haki
inaambatana na wajibu. Amewaomba
viongozi dini kuendelea kuliombea Taifa ili liendelee kuwa na amani na
utangamano, ikiwa ni pamoja na kuwaombea viongozi wa Serikali waweze kutekeleza
vema majukumu ya kuwatumikia Watanzania kwa unyenyekevu na bila upendeleo.
Makamu wa
Rais amempongeza na kumtakia heri Askofu
Wilbroad Henry Kibozi kwa kuwekwa Wakfu na kukabidhiwa kazi ya Askofu Msaidizi
wa Jimbo Kuu la Dodoma ambapo amemuhakikishia Serikali itaendeleza ushirikiano
wa dhati katika utekelezaji wa majukumu yake.
Ibada hiyo
imehudhuriwa na Maaskofu na Mapadre kutoka maeneo mbalimbali nchini, Watawa,
Viongozi wa Dini zingine, Viongozi wa Serikali, Waumini pamoja na wananchi
mbalimbali.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akiagana na Mhashamu Askofu Msaidizi wa Jimbo Kuu Katoliki Dodoma Wilbroad Kibozi mara baada ya ya kumalizika kwa Ibada ya kuwekwa Wakfu Askofu huyo iliyofanyika Kituo Cha Hija Miyuji Mbwanga mkoani Dodoma tarehe 12 Mei 2024.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akiombewa na Mhashamu Askofu Msaidizi wa Jimbo Kuu Katoliki Dodoma Wilbroad Kibozi mara baada ya ya kumalizika kwa Ibada ya kuwekwa Wakfu Askofu huyo iliyofanyika Kituo Cha Hija Miyuji Mbwanga mkoani Dodoma tarehe 12 Mei 2024.
Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki Dodoma Mhashamu Askofu Beatus Kinyaiya akimpongeza Mhashamu Askofu Msaidizi Wilbroad Kibozi mara baada ya kuwekwa Wakfu katika sherehe iliyofanyika Kituo Cha Hija Miyuji Mbwanga mkoani Dodoma tarehe 12 Mei 2024.
Maandamano ya Maaskofu na Mapadre wakati wakiingia katika Kituo Cha Hija Miyuji Mbwanga mkoani Dodoma kushiriki Ibada ya Kuwekwa Wakfu Mhashamu Askofu Msaidizi Wilbroad Kibozi. Tarehe 12 Mei 2024.
Maandamano ya Maaskofu na Mapadre wakati wakiingia katika Kituo Cha Hija Miyuji Mbwanga mkoani Dodoma kushiriki Ibada ya Kuwekwa Wakfu Mhashamu Askofu Msaidizi Wilbroad Kibozi. Tarehe 12 Mei 2024.
Maandamano ya Maaskofu na Mapadre wakati wakiingia katika Kituo Cha Hija Miyuji Mbwanga mkoani Dodoma kushiriki Ibada ya Kuwekwa Wakfu Mhashamu Askofu Msaidizi Wilbroad Kibozi. Tarehe 12 Mei 2024.
0 comments:
Post a Comment