Na Lucas Raphael,Dodoma
Wakala wa Mbegu za kilimo ASA
imewaka wadau mbalimbali katika sekta binafsi wenye uwezo wa kuwekeza katika
kuzalisha Mbegu wazalishe kwani bado kuna uhitaji mkubwa wa Mbegu hapa Nchini.Alisema kwamba serikali imekuwa
ikitumia fedha nyingi kwa ajili ya kuangiza mbegu kutoka nje ya nchini hivyo ni
muhimu kwa wadau mbalimbali kujitokeza kuwekeza kwenye eneo hilo.
“Wakala wa Asa wanamahitaji
makubwa ya mbegu kwani wanaitaji kiasi kikubwa na cha kutosha cha mbegu hivyo
ni muhimu kuwashirikisha wadau ili kuzalisha mbegu bora ili kuwepo na akiba ya
kutosha ili serikali kupitia wakala wasiangize mbegu kutoka nje ya
nchi.”alisema Dkt Kashenge
Dkt. Sophia Kashenge alisema
Wakala umejionea hali ya Shamba hilo na kumwanga sifa na ubora wa mbegu ya Alizeti iliyorolewa
na ASA na kuzalishwa na Saccos hiyo.
Alisema hali ya Mbegu ni nzuri na
ipo katika hatua ya kukomaa huku ikiendelea kutunzwa vizuri na kikundi hicho
cha vijana waliopo kwenye mpango wa BBT.
Dkt. Sophia alisema moja ya
malengo ya ASA ni kufanya kazi na sekta binafsi ili kuongeza uzalishaji wa
mbegu nchini na SACCOS hiyo ya vijana wa BBT ni sekta binafsi muhimu
inayohusisha vijana zaidi ya 260 wakiwemo wanawake takriban 80. Wakala umeingia
nao makubaliano ya kuzalisha mbegu ya Alizeti aina ya Record hekta 300.
Aliongeza kuwa katika makundi
hayo ya BBT kundi la Chinangali Dodoma linazalisha Mbegu za alizeti hekta 300
huku kundi jingine la BBT wanazalisha mbegu katika shamba la Mwele Tanga
wakizalisha mbegu bora ya mahindi hekta 40.
Aidha Mwenyekiti wa Saccos hiyo
Dismas Massage alisema Mbegu hiyo ya Alizeti inaendelea vizuri
Alisema Wakala wa Mbegu za kilimo
ASA ni Taasisi ya Serikali hivyo kama Vijana watahakikisha wanafanya kazi
vizuri ili kuendelea kuaminiwa na Serikali na jamii kwa ujumla.
Alisema katika Shamba hilo lenye
ukubwa wa ekari 300 matarajio yao ni uvunaji Tani 100
Aliwashukuru Wakala wa Mbegu za
kilimo ASA Kwa kuwaamini hasa ikiwa ni mara ya kwanza kufanya kazi hiyo licha
ya kuendesha kilimo hicho cha Mbegu chini ya uangalizi wa wataalam wa Kilimo
kutoka ASA
Alisema matarajio ya Saccos hiyo
nikufanya vizuri katika sekta ya kilimo cha Uzalishaji wa Mbegu Nchini Ili
kuongeza mchango katika upatikanaji wa Mbegu bora za kilimo.
mwisho
MAELEZO KATIKA PICHA
Dkt,Sophia kashenge mtendaji Mkuu wa ASA akiwa
na Mkurugenzi wa Uzalishaji Dkt,Justin Ringo, aliyevaa shat jeupe la mikono
mirefu ni Dismas Masawe mwenyekiti wa
Saccos hiyona huyo mwingine ni makamu
wake wa Saccos ya vijana bbt katika Shamba la mradi Chinangali Dodoma
0 comments:
Post a Comment