Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Angellah Kairuki (Mb) akikagua eneo ambalo lilifanyika zoezi la kufukuza tembo kuwarudisha hifadhini katika Wilaya ya Mbarali Mkoani Mbeya leo Mei 9,2024.
Baadhi ya tembo walioondolewa katika maeneo ya wananchi na kurudishwa hifadhini Wilayani Mbarali, Mkoani Mbeya leo Mei 9,2024.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Angellah Kairuki akizungumza na wananchi wakati wa uzinduzi wa zoezi la kuondoa tembo kwenye maeneo ya wananchi, Wilaya uya Mbarali Mkoani Mbeya leo Mei 9,2024.
Baadhi ya wananchi wakimsikiliza Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Angellah Kairuki (Mb) (hayupo pichani) wakati wa uzinduzi wa zoezi la kuondoa tembo kwenye maeneo ya wananchi, Wilaya uya Mbarali Mkoani Mbeya leo Mei 9,2024.
Serikali kupitia Wizara ya
Maliasili na Utalii imedhamiria kutatua
changamoto ya migongano baina ya binadamu na wanyamapori huku ikisisitiza kuwa katika bajeti
ya mwaka wa fedha 2024/2025
imeweka kipaumbele katika kutatua
changamoto hiyo.
Hayo yamesemwa na Waziri wa
Maliasili na Utalii, Mhe. Angellah Kairuki (Mb) wakati wa zoezi la kuwarudisha
tembo hifadhini lililofanyika Wilaya ya Mbarali Mkoani Mbeya leo Mei 9,2024.
"Tumefanikiwa kuwarudisha
hifadhini tembo takriban 61 na leo tumefukuza tembo 18" Mhe. Kairuki
amesisitiza.
Amesema hiyo inathibitisha
umakini wa Serikali ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kujali usalama wa
maisha ya wananchi na mali zao na uhifadhi wa rasilimali
za wanyamapori na misitu.
Waziri Kairuki amesisitiza kuwa
Serikali itafanya kila liwezekanalo kutatua
changamoto za wanyamapori wakali na waharibifu nchini hususan tembo, Simba
fisi madoa, chui, mamba, kiboko, nyani na tumbili.
"Tutaendelea kuchukua
hatua kwa mujibu wa kila aina ya wanyama na mikakati ya wanyama husika"
amesisitiza.
Amesema zoezi hilo la kufukuza tembo kwa kutumia
helikopta limeambatana na kufunga mikanda ya mawasiliano kwa tembo
viongozi wa makundi mbalimbali ambapo
mpaka sasa imeshafungwa mikanda miwili lakini zoezi litamalizia kwa mkanda wa
tatu.
Pia, amesema Rais Samia ameelekeza kwamba wananchi
walioathirika na wanyamapori wakali na waharibifu walipwe kifuta jasho/machozi katika
vijiji vya Igunda , Rujewa, Mapogoro,
Mlungu, lwalanje,Vikaye, Nyeregete, Manyenga na Mwanavala.
Aidha, Mhe. Kairuki
amezielekeza Taasisi za TANAPA, TAWA na TFS kuendelea kutoa elimu ya uhifadhi
mazingira na namna ya kujikinga na wanyamapori wakali na waharibifu pindi
wanapovamia makazi yao.
Mkutano huo umehudhuriwa na
Watendaji, Maafisa Waandamizi na Viongozi
mbalimbali kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii,TAWA, TAWIRI, TANAPA, TFS,
viongozi wa Chama
pamoja na wananchi.
0 comments:
Post a Comment