Afisa Uhusiano wa Shirika la Umeme Tanesco, Wilaya ya Kigamboni Bi. Tumaini Mahwaya alitambulisha huduma hiyo kwa kuelezea umuhimu wa kutumia huduma mbali mbali za kimtandao zinazotolewa na shirika la Umeme huku akiainisha uokoaji wa mda na fedha zinazoweza kutumika kutoka sehemu ulipo kwenda kwenye ofisi za Wilaya.
Shirika la umeme TANESCO Wilaya ya Kigamboni limeendelea kutoa elimu kwa wananchi wa mtaa wa Lingato kata ya Kisarawe II ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa kampeni waliyoianzisha mapema wiki hii waliyoitambulisha kama "Huduma Mtaani kwako"
Revocatus Maangiri fundi kutoka TANESCO leo Mei 29,2024 ametoa elimu ya namna ambavyo watumiaji wa umeme wanaweza kukabiliana na wananchi wasio waaminifu wanaojitambulisha kwao kama mafundi au watumishi kutoka tanesco wanaoweza kutumia fursa ya kutokujua namna ya upatikanaji wa huduma ya umeme na kuwatapeli.
Aidha Maangiri alitoa elimu ya namna bora ya kutumia vifaa vya umeme ili kuepusha majanga ya moto yanayoweza sababishwa na matumizi mabaya ya vifaa hivyo huku akiwatahadharisha kutumia wakandarasi waliothibitishwa na shirika la umeme kwa ajili ya kutengeneza mfumo wa mtandao wa umeme majumbani.
Naye Isihaka Kita fundi kutoka TANESCO alitambulisha huduma mpya ya kidigitali inayomuwezesha mwananchi kufanya maombi ya umeme na ufatiliaji wa hatua iliyofikiwa ya maombi ya kupatiwa huduma akiwa nyumbani.
Aidha kwa mteja ambaye hana simu janja namba inayotumika kuomba umeme kidigital ni *152*00# huku ikimtaka mteja kufatilia hatua zinafuata kukamilisha maombi yake, na kwa mteja mwenye simu janja atapaswa kuwa na namba ya NIDA itakayomuwezesha kupakua "Ni-konect App" na kuendelea na hatua zinazofuata za kuomba huduma ya kuunganishwa na umeme.
0 comments:
Post a Comment