Shirika la umeme TANESCO Wilaya ya Kigamboni imeanzisha kampeni ya mtaa kwa mtaa inayotambulika kama "Huduma Mtaani kwako "ikiwa na lengo la kutoa elimu kwa watumiaji wahuduma za umeme, upatikanaji wa umeme na huduma zote zinaotolewa na shirika hilo.
Akizungumza mara baada ya kuwasili eneo la mwasonga center lililopo kata ya Kisarawe II, Afisa uhusiano wilaya ya kigamboni Bi. Tumaini Mahwaya alitambulisha huduma hiyo kwa kuelezea umuhimu wa kutumia huduma mbali mbali za kimtandao zinazotolewa na shirika la Umeme huku akiainisha uokoaji wa mda na fedha zinazoweza kutumika kutoka sehemu ulipo kwenda kwenye ofisi za Wilaya.
Aidha bi Tumaini ametoa elimu kwa wananchi namna wanavyoweza kutumia namba ya huduma kwa wateja kwa lengo la kutoa taarifa ya changamoto wanazokabiliana nazo ikiwemo itilafu ya umeme katika maeneo yao.
Naye Afisa wa huduma kwa wateja Ndg. Godwin Marandu ametoa rai kwa wananchi kutoa taarifa za uhalifu kwa vyombo vya ulinzi hasa kwa wale wasio na nia njema kwa shirika na wanaojihusisha na uharibifu wa miundo mbinu ya usambazaji wa nishati ya umeme sambamba na wezi wa vifaa.
Kwa Wilaya ya Kigamboni kwa upande wa utekelezaji wa miradi ya kimkakati, utekelezaji unafanyika kwa awamu kulingana na mahitaji ya wananchi na kwa maendeleo ya wilaya.
Kwa upande wa Kata ya Mwasonga Answary Abdallah ambaye ni Msimamizi wa utekelezaji wa miradi Kigamboni amesema.
"TANESCO inatekeleza miradi hiyo kwa kutumia vifaa bora na vya kisasa ikiwemo utumiaji wa nguzo za zege ili kuepuka uharibifu wa miundo mbinu ya mara kwa mara kutokana na maji na uchomaji wa moto kwa nguzo za mbao".
Aidha ofisi ya TANESCO wilaya ya kigamboni inawaomba wananchi wa Mwasonga kutoa ushirikiano katika utekelezaji wa miradi ili kuleta ufanisi....
0 comments:
Post a Comment