Nafasi Ya Matangazo

May 22, 2024

Naibu Waziri wa Ujenzi Mhandisi, Godfrey Kasekenya amesema Serikali imeanza maandalizi ya kufanya upembuzi yakinifu na usanifu wa kina katika utekelezaji wa ujenzi wa barabara ya Mwembe-Mbaga iliyoko Same Mkoani Kilimanjaro.

Mhe.Kasekenya ameyasema hayo leo Bungeni jijini Dodoma wakati akijibu Swali la Mbunge wa Jimbo la Same Magharibi Mhe. David Mathayo David aliyetaka kujua ni lini barabara ya Mwembe-Mbaga hadi Same itafanyiwa upembuzi yakinifu na usanifu wa kina kwa ajili ya ujenzi wa kiwango cha lami.

 “Mhe. Spika,tayari Serikali imeshaanza taratibu  za manunuzi ya kumpata  Mhandisi  Mshauri kwa ajili ya kazi ya  upembuzi yakinifu na usanifu wa kina wa barabara ya Mwembe- Mbaga hadi Mamba yenye urefu wa kilometa 90.19 katika mwaka wa fedha 2024-2025”, amesema Mhandisi Kasekenya.

Mbunge huyo wa Same Magharibi amezungumzia umuhimu wa barabara hiyo kwa uchumi wa wilaya ya Same na mkoa wa Kilimanjaro kwa ujumla kwa kuwa inapita maeneo yenye uzalishaji mkubwa wa mazao ya chakula na biashara.

Posted by MROKI On Wednesday, May 22, 2024 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo