Nafasi Ya Matangazo

May 05, 2024




Maneno hayo pamoja na ushauri juu ya mienendo ya kiutendaji miongoni mwa Maafisa RasilimaliWatu yamesemwa na Naibu Waziri wa Utumishi na Utawala Bora Ndg. Ridhiwani Kikwete J. alipokuwa anafunga Mkutano wa 11 wa wanachama wa Chama Cha Maafisa Tawala na Rasilimali Watu (AAPAM) uliofanyika katika Ukumbi wa AICC , jijini Arusha.

Naibu Waziri Kikwete, ameelekeza Maafisa hao kuendelea kutumia mifumo ya utendaji kazi ili kuwezesha  haki na wajibu  kutolewa kwa watumishi wa umma. Akizungumza na watumishi hao katika siku ya mwisho ya Mkutano huo wa siku tatu, Ndugu Kikwete aliwakumbusha watumishi hao mifumo mbalimbali iliyokwisha tengenezwa kuwezesha watumishi kukopa, kuhama na kupima utendaji kazi.

Katika hali nyengine , Naibu Waziri Kikwete amewaonya Maafisa hao juu ya tabia inayoendelea ya kutowatendea vyema watumishi wenzao wanaowaongoza.  Naibu Waziri ameonya juu ya roho mbaya walizonazo baadhi ya Watendaji hao akitoa mfano wa Rorya na taratibu za upandishaji madaraja.

#KaziInaendelea #AAPAMTanzania
#WatendajiBadilikeni
Posted by MROKI On Sunday, May 05, 2024 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo