Nafasi Ya Matangazo

May 23, 2024











Baraza la madiwani wilaya ya Kigamboni, Mkoani Dar es Salaam, limewasilisha taarifa za kata kwa robo ya tatu  kwa mwaka wa fedha 2023/2024. 

Katika kikao hiko Madiwani waliwaslisha taarifa za utekelezaji wa shughuli mbali mbali katika kata zao huku wakiainisha changamoto na namna wanavyokabiliana kuzitatua ili kuleta ustawi kwa wananchi katika maeneo husika. 

Diwani wa kata ya kibada Mhe. Mzuri Sambo alielezea changamoto ya miundo mbinu hususani ya bara bara inayopelekea kukwamisha baadhi ya shughuli za maendeleo katika maeneo kadhaa ndani ya kata hiyo¹

Naye Diwani wa kata ya Vijibweni Mhe. Zacharia Mkundi amemuomba Mkurugenzi mtendaji kuangalia namna anavyoweza kuelekeza fedha kwenye ukarabati wa bara bara ikiwa utekelezaji wa suala hilo hautathiri uendelezaji wa  shughuli za maendeleo ndani ya Manispaa. 

Hata hivyo swala la uharibifu wa bara bara limekua  changamoto kwa kata zote za wilaya ya kigamboni kutokana na mvua zilizonyesha huku likimuinua mkurugenzi mtendaji na kaimu Meneja wa TARURA katika kueleza namna mipango ndani ya wilaya inavyotekelezwa kwenye utatuzi wa changamoto hiyo. 

Akizungumza Mkurugenzi mtendaji wa Manispaa ya Kigamboni Ndg Erasto Kiwale alisema tayari  wamejipanga kuendeleza ujenzi wa bara bara hizo huku wakiwa tayari wameandaa kikao kitakachoketi kujadili na kuchanganua namna watavyo anza utekelezaji kwa maeneo yatakavyoainishwa. 

Aidha Mkurugenzi Kiwale amewataka watendaji wa kata kuweka vipaumbele katika utekelezaji wa majukumu katika maeneo yao huku akiwaonya kuacha kusubiri maelekezo ya  nini wafanye kutoka ngazi ya Manispaa. 

Sambamba na hilo Kaimu Meneja TARURA Enginia Edger Tumsifu amesema tayari jitihada za kufanya ukarabati kwa maeneo korofi zinaendele huku akiainisha kuanzishwa kwa ujenzi wa bara bara zinazounganisha kibada na kisarawe II na ameainisha  hatua zilizofikiwa ikiwemo kukamilika kwa mchakato wa kumpata mkandarasi wa ujenzi wa barabara hizo.
Posted by MROKI On Thursday, May 23, 2024 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo